ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 14, 2016

MVUA YAUA MTOTO JIJINI MWANZA: HALI TETE KWA BARABARA ZA MWANZA

Mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa nne jijini hapa leo, imesababisha kifo cha mwanafunzi na uharibifu wa mali zenye thamani ya mamilioni ya fedha.

Wananchi wamedai kuwa mvua hiyo, iliyonyesha kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri, haijawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne iliyopita.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabatini, Ntobi Ntobi pamoja na kaimu kamanda wa kikosi cha Zimamoto jijini Mwanza, Hamidu Nguya walithibitisha kutokea kwa kifo cha mtoto huyo, Jenipher Joseph (6), aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini.

Kamanda Nguya alisema mtoto huyo alisombwa na maji na baba yake, James Joseph walipoteleza na kuangukia mtoni wakati wakivuka daraja la Mto Mirongo uliokuwa umefurika.

Mvua Yauwa Mtoto 1 Mwanza

Fuatilia taarifa hii iliyoandaliwa na Star TV. Mwanza.


Mkazi wa Mabatini jijini Mwanza akijiokoa kwa
Mkazi wa Mabatini jijini Mwanza akijiokoa kwa kupanda juu ya bati, baada ya eneo lao kukumbwa na mafuriko ya maji kutokana na mvua iliyonyesha jana jijini humo.  Picha na Michael Jamson.
Huku wengine wakivuka katika eneo la daraja maarufu kama Daraja la Wakoma lililopo barabara ya uhuru wilayani Nyamagana jijini hapa, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji pamoja na wadau wa Idara ya maji safi na maji taka Mwanza MWAUWASA wanaendelea na juhudi ya msaka mtoto aliyezama.
Miongoni mwa waliopoteza mali ni pamoja na Juma Said, mmiliki wa duka la vifaa vya shule na ofisi zenye thamani ya zaidi ya Sh7.5 milioni.

Licha ya ubovu wa miundombinu, eneo la Mabatini hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na ujenzi holela uliobana kingo za Mto Mirongo.

Hadi saa wakati tunatoka eneo la tukio, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa kikiendelea na juhudi za uokoaji na kutafuta miili ya watu wanaodhaniwa kuwa wamesombwa na mafuriko hayo.


Huu mchanga na tope umejikita hapa na kusababisha barabara kupitia kwa shida.
Kingine ambacho kimekuwa changamoto kubwa kwa watendaji wa sekta mbalimbali za uokoaji ni suala la ukosefu wa vitendea kazi., hakukuwa na vitendea kazi madhubuti vya uokoaji zaidi ya fimbo na miti kwaajili ya kuzibua taka zinazojikita kwenye kingo za daraja hilo.
Hali tete juhudi zimekwama.....
Mitaani nako si salama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.