ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 9, 2016

AKILI MKICHWA.

Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia ''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili hivyo hivyo"
Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule ''Wanafunzi wakakubali afu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.
Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia.
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake afu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi. Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu moyoni usiowapenda. 

Kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.? Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokuwa moyoni. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri.
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe mana ni moja ya virutubisho vya moyo wako. Hata Mungu anasema wasamehe wale waliokukosea ili upate amani na baraka moyoni mwako. Nawatakia siku njema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.