ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 8, 2015

TANGAZO LA KAZI

Kampuni ya NOFO ya jijini Dar es Salaam, inayojihusisha na uchapishaji na uuzaji wa vitabu vya hadithi za watoto, inatangaza nafasi kumi za kazi ya afisa masoko. Wenye sifa zifuatazo watume maombi kupitia baruapepe ndejarini@gmail.com kwenda kwa GENERAL MANAGER, NOFO, DSM
(1)    Shahadaya kwanza au stashahada ya juu ya biashara katika masoko
(2)    Uelewa mzuri na ueledi wa kuimarisha na kupanua wigo wa masoko
(3)    Ari na moyo wa kufikia malengo uliyo wekewa
(4)    Uwezo wa kujieleza vizuri mbele ya watu wengi

Mwisho wa kupokelewa kwa

JANET MBENE AKABIDHI VITANDA VYA KUJIFUNGULIA VYA THAMANI YA MILIONI 30 ILEJE.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi Vitanda vya Kujifungulia Katibu wa CCMwilaya ya Ileje kwa ajili ya Hospitali za wilaya hiyo.
Mafundi wa Hospital wakiunganisha kitanda cha kujifunguliwa kilicholetwa na Mh Janet Mben kwa ajili  ya hospitalai za ieleje.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene,akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika hospital ambavyo avimetolewa na Karemjee Foundation kwa ajili ya Hospital ya Ileje.
Mganga mkuu wa Wilaya ya ilje akiangalaia sehemu ya msaada wa vitanda uliotolewa na Janet Mbene.

JK AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA YENYE UREFU WA KILOMETA 60 MKOANI LINDI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.
Rais Kikwete akimshukuru  Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma  Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na   Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na  Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho  Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akiwa sambama na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh.Mwantumu Mahiza.
Wananchi kutoka kijiji cha Marendego na vijiji vyake wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu –Somanga yenye urefu wa kilometa 6,inayojengwa na Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa mfuk wa Kuwait pamoja na Opec.Katika unziduzi huo viongozi mbalimbali wa chama na serikal,viongozi wa dini pamoja na watu wengine walishiriki kushuhudia tukio hilo adhimu hapa nchini.
Wananchi wakifuatilia tukio hilo.
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ya Ndundu -Somanga yenye urefu wa kilometa 60
Wananchi wakifurahia ufunguzi wa barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.


PICHA NA MICHUZI JR-LINDI

Friday, August 7, 2015

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA APETA KURA ZA MAONI UDIWANI CHADEMA, SASA KUSUBIRI KURA ZA UBUNGE.

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala al-maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu.

SHINYANGA
MWANDISHI wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.

Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.
Kulia ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala al-maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi” anapokuwa kazini kikazi zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Sambamba na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.

Kwa upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.



Kwa sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.

SERIKALI YAUTAKA MGODI WA BULYANHULU KUWALIPA FIDIA WAATHIRIKA WA SUMU


Na Emmanuel Mlelekwa
KAHAMA
Baraza la hifadhi ya mazingira la Taifa NEMC limethibitisha kuwa mgodi wa uchimbaji madini wa ACACIA Bulyanhulu ulioko wilayani Kahama Mkoani Shinyanga umebainika kuwa na kosa la kushindwa kuzuia Sumu inayotumika kusafishia Dhahabu na kupelekea athari katika jamii inayozunguka mgodi pamoja na viumbe hai.

Akitoa ripoti ya uchunguzi wa kimaabara   ya NEMC kwa vyombo vya habari mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema kuwa mgodi wa Bulyanhulu ACACIA haukuwa makini katika kuhifadhi sumu hiyo hali ambayo ilipelekea wakazi 130 kupata madhara ya kiafya pamoja na viumbe hai wanaoishi majini.

Amesema kuwa mnamo January 8 Mwaka huu sumu hiyo aina ya Cynide ilisambaa kwenye mashamba ya wakulima kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyobomoa ukingo wa ukuta unaohifadhi maji yenye sumu hiyo na kuepelekea kiwango kikubwa cha sumu kusambaa kwenye maeneo ya mashamba ya wakulima.

Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo serikali kupitia ripoti ya NEMC imeutaka mgodi huo kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha Kakola namba 9 ambao waliathiriwa na sumu hiyo ambao baada ya tukio hilo kutokea walitakiwa kutotumia maeneo yao ikiwemo kilimo kwa kwa kipindi cha mwaka mzima na kupelekea kukabiliwa na tatizo la njaa.

Hata hivyo mkuu wa wilaya amesema kuwa ni lazima wakazi wa eneo hilo walipwe fidia ili waweze kununua chakula kwani serikali ilikuwa bado inasubiria ripoti ya NEMC ambayo imetolewa na kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi na udhibiti wa mazingira mgodi inatakiwa ufanye hivyo.

Kauli hiyo imekuja  kufuatia wakazi wa kijiji cha Kakola Namba 9 kulalamika mbele ya waandishi wahabari kuwa mgodi wa Bulyanhulu wameshindwa kuwalipa fidia kutokana na uharibifu uliotokana na sumu hiyo jambo ambalo limechangia wakazi wa eneo hilo kukabiliwa na uhaba wa chakula na madhara mbalimbali kiafya.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIGAE MKOANI MBEYA.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Janet Mbene,akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akizungumza, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Marmo and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani Mbeya hivi karibuni.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akizungumza, mmoja waviongozi wa kampuni ya Marmo and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani mbeaya hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Janet Mbene,akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janet Mbene, akitembelea sehemu ya kiwanda cha Marmo anda Granito Mines

ADC YAFANYA MKUTANO WA HADHARA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA WA URAIS KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli Dar es Salaam jana. 
 Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
 Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
  Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli jana.
Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu. 

DKT BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFEREJI MPYA WA SUEZ ISIMAILIA AGOSTI 06, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6, 2015 jijini Ismailia. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFEREJI MPYA WA SUEZ
ISIMAILIA AGOSTI 06, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana ameiwakilisha Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha mabara ya Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita "zawadi mpya kwa Dunia" unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri ambayo kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana na meli zitakazopita katika mfereji huo.

Mradi wa ujenzi wa Mfereji huu mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa kukamilika baada ya miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni Nane ambazo zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa kwa Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli kusimama ili kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila kuathiri upande mwingine.
Sherehe hizo za aina yake zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata kuripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa fursa mpya za maendeleo zipo Afrika.

Sherehe hizo za  aina yake zilipambwa na maonesho ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji mpya wa Suez huku zingine zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi bendera ya Misri, zingine zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.

Katika tukio hilo la kuathimisha tukio hilo la kihistoria   serikali ya Misri ilitangaza kuwa  siku hiyo ni ya mapumziko huku ulinzi mkali ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya nchi hiyo huku jiji la Cairo walipofikia  viongozi mbalimbali wa kimataifa likiwa chini ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote muhimu. 

Barabara ya kwenda eneo la Islamelia zilikofanyika sherehe hizo ilifungwa kwa siku nzima,  walioruhusiwa kupita  ni viongiozi na wageni mbalimbali  waalikwa waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.

 Rais wa Misri Abdel  Fatah  Sisi alisema kufunguliwa kwa Mfereji  ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na kueleza kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na kufungua fursa zaidi kwa mataifa  duniani.

Katika moja ya matukio ya  uzinduzi huo Rais Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo walisafiri katika meli za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri akivalia mavazi maalumu ya kijeshi akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa miaka tisa aliyevalia kijeshi na kupeperusha bendera ya  Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa mfereji huo.

Shughuli  ilimazika usiku  kwa  maonesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri  na kuhudhuriwa na viongozi na wageni wote waalikwa.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Cairo Misri Agosti 7, 2015

JEMBE FM YAZIDI KUNAKSHI MAONESHO YA NANE NANE MWANZA KIMAWASILIANO.

Oxy Okeleky (kulia) akifanya mahojiano na mmoja wa wadau wajasiliamali wanaofanya shughuli ndani ya maonesho ya Nane nane ndani ya viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Ufugaji na Kilimo umehusishwa ndani ya maonesho haya.
Kilimo kwa kutumia jembe la kukukotwa na ng'ombe.
Chriss The Dj toka Jembe Fm akiwa pamoja na Okeleky wakishangaa mashine ya kupukuchua mahindi katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Ufugaji wa samaki.
Ufugaji bora wa samaki na kware, ufugaji mseto samaki.
Ufugaji bora.
Mboga mboga.
Nyanya.
Shamba la mfano kilimo cha Mpunga.
Kabichi na aina zake.
Zao la pamba na wadudu waharibifu.
Kilimo cha nafaka, na changamoto zake ikiwa ni sanjari na elimu ya kukabiliana nazo.
Mayai ya Kware, toka katika banda la Faith Poultry Fam.
Moja ya huduma wanazozitoa ni Kuzalisha na kukuza vifaranga vya Kware na mayai.
Kuuza vifaranga vya kuku wa kienyeji na chotara.
Kuuza majarida na vitabu vinavyoeleza ufugaji bora wa Kware.
Kutotolesha mayai ya kuku, kanga, kware na bata mzinga.
Familia ya Jembe Fm na ukuaji wake.
Kutoka TBL hii ni Zagamba.
Matrekta.
Kutoka Kona ya Bujora Kisesa hawa ni vijana wapenzi wa kipindi cha  ** KAZI NA NGOMA**
Mkurugenzi wa Jembe FM Dr. Sebastian Ndege (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa Viwanja Kisesa Isangijo vilivyopo kilimita 20 kutoka Mwanza mjini Barabara ya Musoma, pindi walipotembelea studio za Jembe Fm Mwanza.

Kutoka kushoto ni Damas Mwakindingo ambaye  ni Afisa Ardhi Mteule Magu, Ally Msoya Mkurugenzi Landspecs Developer LTD na kulia ni Simon Chuwa ambaye ni Technical Manager wa Landspecs Developer LTD.
PAMOJA SANA.