ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 14, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KIUCHUMI NA MAENDELEO WA MISRI (EGYPT THE FUTURE).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati akiwa katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawekezaji wa Misri wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Viwanja Wilayani Mkuranga, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo leo, Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri, alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Misri, Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya mkutano huo, uliofanyika jana Machi 13, 2015 mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake Wawekezaji wa Misri wanaoataka kuwekeza katika Sekta ya Viwanda Wilayani Mkuranga, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR



 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KIUCHUMI NA MAENDELEO WA MISRI (EGYPT THE FUTURE)
SHARM EL SHEIKH, MISRI MACHI 14, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Machi 13, 2015 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi na Maendeleo nchini Misri. Mkutano huo umeandaliwa na Rais wa Misri Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi na umehudhuriwa na viongozi karibu wote kutoka katika nchi za Kiarabu, marais na viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali za Afrika pamoja na wakuu wa vyombo mbalimbali vya Kimataifa akiwemo pia Waziri wa Mmabo ya Nje wa Marekani John Kerry.

Akizungumza katika Mkutano huo, Rais wa Misri aliueleza ulimwengu kuwa Misri imepita jaribio kubwa na sasa iko imara tayari kusonga mbele hivyo wale wote walio na nia ya kuwekeza nchini Misri wafanye hivyo kwa kuwa serikali yake itashirikiana nao katika kuwalinda wao na mali zao. Pia Rais Sisi alifafanua kuwa, nchi yake inarejesha heshima yake iliyokuwa nayo zamani kutokana na mchango wake katika Umoja wa nchi za Kiarabu huku pia akisisitiza kuwa Misri sasa inarejea Afrika ambako anatambua kuna ndugu wa dhati.

Akihutubia mkutano huo Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal aliishukuru Misri kwa kuialika Tanzania kuhudhuria mkutano huo na akafafanua kuwa Tanzania inafurahia uamuzi wa Misri wa kujijenga upya huku ikikumbuka historia ya kutaka kujiwekea nafasi yake katika Afrika na katika nchi za Kiarabu.

“Mheshimiwa Rais, uitishaji wako wa mkutano huu mkubwa ni kiashirio kuwa sasa Misri inajijenga upya na kwamba inarejesha heshima yake katika Bara la Afrika, Nchi za Kiarabu na Dunia kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Dkt Bilal na kuendelea kuwa:

“Tunakupongeza kwa uongozi thabiti uliouonesha hadi sasa ambapo Misri inaonekana kuwa imara na thabiti. Uhusiano wetu ni wa kihistoria hivyo Tanzania inakupongeza na inaahidi kushirikiana nanyi katika ujenzi mpya wa Taifa lenu.”

Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alitumia nafasi hiyo kuueleza mkutano huo kuwa eneo ilipo Misri linaunganisha Afrika, Nchi za Kiarabu na Ulaya na Tanzania nayo iko katika eneo la kitajiri kijiografia ambapo ukiwekeza nchini Tanzania unakuwa unapata fursa za ziada za kuwekeza katika nchi za Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika.

 “Ukiwekeza Tanzania utakuwa na uhakika wa soko la watu wasiopungua milioni 400 na nchi zetu ni lango la nchi zipatazo nane ambazo hazina bahari,” mheshimiwa Makamu wa Rais alisema na kufafanua kuwa Tanzania inakaribisha wawekezaji kama ambavyo Misri inafanya na zaidi akaeleza kuwa fursa za uwekezaji Tanzania ni nyingi na hasa sasa ambapo tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Katika mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na Mheshimiwa Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na kuzungumza naye na kisha kuhudhuria mada ya kiuchumi iliyowasilishwa na Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake wanarejea nyumbani kesho tayari kuendelea na majukumu mengine ya Kitaifa.
 Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
           Sharm el Sheikh, Machi 14, 2015

KOCHA SYLVESTER MASH AFARIKI DUNIA

Enzi za uhai wake Marehemu Syvester Mash (kushoto) akipewa maelekezo toka kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen 
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako ndiko alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu. 

Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Chama cha soka mkoawa Mwanza MZFA Nasib Mabrouk amethibitisha kutokea kwa msiba huo akisema kuwa ni kipindi zaidi ya mwaka sasa kocha Marsh amekuwa akiugulia na sasa Mwenyezi Mungu ameamua kumpumzisha hivyo amewataka wapenzi wa soka kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu huku akisema kuwa wasubiri taratibu za mazishi na harakati mbalimbali ambazo zitatangazwa baadaye leo mara baada ya kukamilika kwa taarifa kamili.

Zaidi tukutane ndani ya Sports Xtra Clouds Fm kwa taarifa kamili.


R.I.P SYLVESTER MASH

Friday, March 13, 2015

PPF MKOA WA MWANZA YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 NA MABATI 100

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisalimiana na meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Mesharck Bandawe pindi alipowasili jana Kahma mkoani Shinyanga kutoa pole kwa waathirika wa mvua zilizoambatana na upepo eneo la Mwakata wilayani humo.
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali inatafuta fedha za kujenga nyumba 468 mpya za kisasa na kukarabati nyumba zilizoezuliwa na upepo katika eneo la Mwakata huko Kahama mkoani Shinyanga pamoja na kuendelea kuhudumia waathrika wote kwa chakula, malazi na dawa hadi watakapopata makazi bora ya kudumu. 
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe akitoa taarifa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, Mabati 112 na mifuko ya simenti 100 msaada wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni tatu za kitanzania.
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) akikabidhi msaada wa simenti na mabati kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
Jumla ya mabati 112 yamekabidhiwa kama sehemu ya msaada.
Nayo mifuko 100 ya simenti ni sehemu ya msaada toka PPF.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kushoto) akitoa shukurani kwa PPF kupitia Meneja wake Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kulia) mara baada ya kukabidhiwa msaada wa simenti na mabati kwaajili ya wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
PPF. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa na wilaya kutembelea maeneo ya kata za wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi. 
Ukuta umeanguka paa liko mashakani.
Hali tete.
Salaaam .....poleni. 
RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi.


Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha duni wanayoishi watu hao.


Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa kuwajengea nyumba hizo.


Pia, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda mfupi na hakuna uchakachuaji.


Aliwataka viongozi mkoani Shinyanga kuhakikisha ujenzi huo hautangazwi na kuagiza JKT kwenda kwenye eneo hilo kufanya tathmini ya ujenzi huo ili uanze mara moja.


Rais Kikwete aliwatoa wasiwasi wananchi wa Mwakata waliokumbwa na tatizo hilo kwamba Serikali itahakikisha wote wamepata chakula hadi mwisho watakapolima na kupata mavuno na tukio hilo wasilihusishe na imani za kishirikina.


Alisema mvua hizo ni za kawaida ambazo hutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na si ushirikina hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuwa na hisia hizo lakini wasilichukulie kwa uzito swala la ushirikina wakatafuta mchawi wa mvua hiyo


Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga alimwambia Rais Kikwete kwamba mvua hiyo licha ya kuua watu 47 pia imeharibu mazao hekari 2,332 pamoja na visima 53 vya maji ya kunywa.


Rufunga alisema mpaka kufikia sasa wahisani mbalimbali wamechangia kwenye tukio hilo Sh64 milioni pamoja na tani 63 za unga wa sembe pamoja na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu yakiwamo mabati zaidi ya 1,000

MKAZI WA KOROGWE, TANGA AIBUKA MSHINDI WA MTOKO WA MBUGANI KWENYE FAINALI YA TUTOKE NA SERENGETI

Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium, Bw.Rugambo Rodney, wa pili kulia, akionyesha namba ya simu ya mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti, ambapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe, Tanga aliibuka mshindi.Msimamizi toka PWC, Golder Kamuzora na (wa pili kulia), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha,Bw. Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto) Afisa Mauzo toka SBL, Anitha Moshi, (wa kwanza kulia). Droo hiyo iliyofanyika katika baa ya Hongera jijini Dar es salaam.
Mmoja wa washiriki wa droo ya mwisho ya “Tutoke na Serengeti,” Morris Maro wa pili toka kulia akibonyeza kitufe cha laptop kuchezesha droo hiyo wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa "Mtoko wa mbugani" katika kampeni ya Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilifanyika Hongera baa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam amapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe,Tanga aliibuka mshindi. Kwenye picha ni Meneja chapa bia ya Serengeti premium Bw. Rugambo Rodney (wa pili  kushoto), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto), na Getrud Mzava*mteja) aliyeitwa kushuhudia, droo hiyo ikichezeshwa kwa haki ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mateja wa Serengeti Premium Lager, Getrud Mzava ,akitaja namba za simu za mshindi wa mwisho katika droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa Mtoko wa mbugani, ambapo mkazi wa Korogwe,Tanga,Bw.Robert Gabriel aliibuka mshindi wa Mtoko wa Mbugani. Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Bia chapa ya Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney, (wa pili kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti katika droo iliyochezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.Kulia ni Afisa mwandamizi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo.
Kaimu Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Bw. Elihuruma Ngowi akiwahudumia baadhi ya wateja walioshiriki wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho  wa Mtoko wa Mbugani wakati droo hiyo ilipochezeshwa ambapo mkazi wa Korogwe-Tanga,Bw. Robert Gabriel aliibuka mshindi wa mwisho wa shindano hilo,lililofanyika katika Baa ya Hongera-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka SBL wakikonga nyoyo za  washiriki wa Droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa Mbugani” ambapo Bw.Robert Gabriel toka Korogwe-Tanga aliibuka mshindi wa droo hiyo iliyochezeshwa jana katika Baa ya Hongera iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washindi wa shindano la Tutoke na Serengeti, Bw.Godfrey Mpiruka aliyeibuka na zawadi ya Limo Bajaji siku za nyuma akiteta jambo na afisa toka SBL wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya shindano hilo, lililofanyika katika baa ya Hongera iliyopo-Kijitonyama jijini Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI SHARM EL SHEIKH KUHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU MAENDELE NA UCHUMI WA NCHI YA CAIRO MISRI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, jana kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri. Picha na OMR
Mhe. Makamu wa Rais aliwasili jana na kupokelewa na mwenyeji wake.  Akifafanua kuhusu mkutano huo Dkt Bila alisema kuwa ‘’Misri ni wadau wetu katika maendeleo,  uhusiano kuwa mkutano huu utafungua fursa zaidi za uwekezaji baina ya nchi zetu.
Mkutano huo wa siku tatu utafunguliwa baadaye leo na Rais wa Misri Abdel Fahah  Sisi, na kuhudhuriwa na baadhi ya wageni mashuhuri kutoka Mataifa mbalimbali akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry

IT'S FRIDAY AND ITS ON ‪#‎TGIF‬, SKYLIGHT BAND KUKINUKISHA THAI VILLAGE USIKU WA LEO

DSC_0292
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari huku waimbaji wenzake Sony Masamba (katikati) na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Wadau na wapenzi wa muziki wa live na wa kiwango cha juu, wote wanakutana Thai village Masaki, jioni hii kwa burudani safii toka kwa wakali wa town vijana wa Skylight Band.
Karibuni sana tuanze weekend yetu na burudani ya muziki wa Live
Come and experience good music from our young talented singers #‎Aneth‬Kushaba ‪#‎John‬ music & #‎Ashura #‎Sony‬ Masamba #‎Sam Mapenzi bila kumsahau baba lao Joniko Flower mkongwe kwenye burudani ya muziki wa Live...ni balaaaaa na si ya kukosaa.. Hii ni ijumaa ya amsha amshaa# una kila sababu ya kusogea Thai village na bila kusahau Jumapili hii Escape1#

DSC_0285
Vijana wa Skylight Band wakitikisa jukwaa kwa 'style' za aina yake.
DSC_0348
Mashabiki nao hawakubaki nyuma katika miondoko.
DSC_0329
Majembe ya Skylight Band yakijembeka ndani ya kiunga cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Twende sawa......
DSC_0311
Sam Mapenzi aki-'feel' ala za gitaa alipokuwa akifanya Kolabo na Aneth Kushaba AK47 ya wimbo wa Elani wa 'Kookoo' unaobamba kwenye chati za muziki nchini Kenya. Kushoto ni Ashura Kitenge akipiga back vocal.
DSC_0318
Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0341
Ijumaa iliyopita alizaliwa binti mrembo sana Super Model, Neema Mbuya mdau mkubwa wa Skylight Band. Pichani akitoka kuimbiwa wimbo wa 'Happy Birthday' na bendi ya Skylight.
DSC_0333
Birthday Girl Super Model, Neema Mbuya na mashosti zake wakisheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa iliyoangukia akiwa batani Skylight Band na ma-surprise kibao kunogesha siku yake.
DSC_0336
Mmoja wa marafiki wa birthday girl akitaka kumwogesha na kinywaji.
DSC_0338
Mwanadada mrembo na mdau wa Skylight Band akipozi kwa Ukodak.....
DSC_0351
Aneth Kushaba AK47 akisebeneka na shabiki wake back stage.
DSC_0356
Mdau wa Skylight Band Mule mtoto wa Sinza kwa wajanja akipata ukodak na binti mrembo ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0306
Murembo figure namba nane....hapana chezea Skylight Band.

MABOMU YARINDIMA SAA HII MWANZA INSHU NI ILE ILE POLISI NA MACHINGA

Vurugu zimezuka mida hii ya saa 5 asubuhi zikihusisha polisi na machinga wa mkoa wa Mwanza suala ni lile lile, polisi wakijaribu kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wanaojishikiza katika maeneo yasiyoruhusiwa mitaa ya Makoroboi na Lumumba.

Wafanyabiashara wengi kati ya hao walio katika vurugu hizo wamekuwa wakilalama kwa madai ya mkanganyo unaojitokeza kila kukicha kwa kauli za wanasiasa zikipingana na maamuzi ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Halmashauri ikiwaondoa maeneo hayo yasiyo ruhusiwa nao baadhi ya wanasiasa akiwemo Mkuu wa mkoa wa sasa wa Mwanza Mhe. Mlongo naye akiwarudisha kwenye maeneo hayo...... ITAENDELEA  

Thursday, March 12, 2015

WAGANGA 55 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA

MWANZA

JESHI la polisi Mkoani hapa limewashikilia waganga wa jadi 55 wanaodaiwa kupiga ramli chonganishi katika msako unaoendelea katika wilaya zote za Mkoa huu.


Waganga hao wa jadi wamekamatwa kutokana na kutuhumiwa kupiga ramli chonganishi zinazosababisha na kuchochea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na wazee (vikongwe).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola,alisema waganga hao walikamatwa  Machi 6 mwaka huu, katika msako unaondeshwa na jeshi hilo, kuwasaka waganga wasio na vibali vya kufanya kazi hiyo.

Kwa mujibu wa kamanda Mlowola alisema waganga hao walikamatwa wakiwa na nyara mbalimbali za serikali ambazo hawazimiliki kihalali na wamekuwa wakizitumia katika shughuli zao za uganga.

“Waganga wasio na vibali,wanaopiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya ya watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) ambapo amuaji haya yameleta madhara  makubwa na kuchafua taswira ya nchi yetu." alisema Mlowola.

Katika hali ya kushangaza alisema, mmoja wa waganga hao 55 kati yao wanawake wakiwa 18, alikutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi kilo 3, ambayo alikuwa akiitumia kama dawa tiba kwa wateja wake.

kwa mujibu wa Kamanda Mlowola alizitaja nyara walizokutwa nazo kuwa ni ngozi ya samba, mikia ya nyumbu, mikia na pembeza swala, jino la kiboko, korongo, ndege na vinyonga waliokaushwa, yai la mbuni, konokono, kanga na ngozi ya kenge .

Vingine vya ramli chonganishi walivyokutwa navyo waganga hao  ni vibuyu, simbi, visonzo,  sarafu za kale an noti za amani, manyanga, ,fimbo, kioo, vibao, zozo, kengere, njuga, fimbo, kigoda, karatasi za Quran, jiwe mizizi mbalimbali, vyungu, mikuki, mishale, shuka nyeupe, nyekundu na nyeusi.

Alieleza kuwa waganga hao baadhi wamefikishwa mahakamani na wengine bado walikuwa wakiendelea kuhojiwa ambapo alivitaka vyombo vya habari kuelimisha jamii kuhusu mila potofu za imani za kishirikina, kwa kuandika makala za kupinga mila na tamaduni zilizopitwa na wakati.

“Kwa nafasi yenu nawasihi muielimishe jamii,iachane na mila potofu za imani za kishikirikina kuwa viungo vya binadamu (albino) vinauwezo wa kumtajirisha mtu,bali utajiri unatokana na juhudi za mtu kufanya kazi kwa bidii na si viungo vya binadamu,”alisema Mlowola.

HuaweiUnveils “Huawei Watch” at The Mobile World Congress 2015

Powered by Android Wear, the Huawei WatchFeatures a Fully Circular Timeless Design
Barcelona, Spain,March 1, 2015: Huawei continues to break new ground in the wearables space byunveiling today the Huawei Watch, powered by Android Wear™atMobile World Congress (MWC) 2015. The fully circular watch features a 1.4-inch touch-sensitive AMOLED display,scratch-proof sapphire crystal lens, cold-forged stainless steel frame, and comes with a built-in heart ratemonitor and 6-Axis motion sensors. The Huawei Watch is the firstsmartwatch in the Huawei wearable family.

“We have responded to consumers’ requests from around the worldaskingfor a smartwatchfeaturing a timeless design that is trulysmart from within.Through Huawei’scontinued commitment to ‘Make It Possible,’the Huawei Watchdelivers on that promise and gives the consumer a premiumsmartwatch thatis technologically innovative,” said Richard Yu, CEO, Huawei Consumer Business Group. “As the first smartwatch in our expanding lineof premium wearable products,the HuaweiWatch was designed and createdtoenhance and be part of the consumer’s everyday lives.”

Timeless Design
Designed by ateam of experiencedwatchdesigners that have a rich history in creating fashionableand timelesswatches, the attention-to-detail becomes apparent upon first glance as the device boasts a sparkling AMOLED 1.4-inch display at 400 x 400 pixels resolution in 286 ppi at a 10,000:1 high contrast ratio,making it the most vibrant Android Wear smartwatch in the world.

Madeof more than 130 components, Huawei Watch hasa crown, frame and hingebuilt from high-quality and scratch resistant cold-forged stainless steel making it 40 percent harder. With an intuitive 2 o’clock press button, the watch offers the highest levels of control and comfort to the user.The Huawei Watch comes in three stylish colors: gold, silver and black.

Designed with personalizationin mind, more than 40 unique watch faces will be available to choose from, including a full range of watch straps made from differentmaterials,and styles. The Huawei Watchwill come with a magnetic charging station for the users benefit.

Smart Within
Powered byAndroid Wear,receiving SMS, email, calendar, app, and phone call notifications has never been easier or more convenient.Compatiblewithsmartphones running Android 4.3or higher, Huawei Watch boastsa powerful Qualcomm 1.2GHzprocessor for optimal performance,includes4GB of storage,512MB of RAMandBluetooth 4.1. For the sports enthusiast, or just those interested in tracking fitness levels, Huawei Watchfeatures a heart rate monitor sensor, 6-Axis motion sensor, and barometer sensor that automatically detects and tracks in real-time if a user is walking, running, biking, hiking or sleeping. Specifically, users can monitor everything from the number of calories burned, to heart rate, climbing height,steps taken, and distance travelled.

Huawei Health Ecosystem
To encourage consumers to live happier and healthier lives, Huawei is dedicated to building a wearable’s health and lifestyle ecosystem that will help users set goals and track their progress. With exciting partnersincluding Jawbone, theHuawei Health Ecosystem seeks other innovative third-party health and fitness apps that will encourage users to set themselves free.

Availability and Accessories

Huawei Watchwill be available in morethan 20countries includingUnited States, United Kingdom,Argentina, Australia, Brazil, Canada, Denmark, Finland, France, Germany, Hong Kong, Italy, Japan, Norway, Philippines, Russia, Singapore, South Korea, Spain, Sweden, Switzerland, United Arab Emirates. Exact availability and pricing will be announced at a future date in each of the local markets.