ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 18, 2015

HARAKATI ENDELEVU ZA KIKUNDI CHA “BUKOBA MPYA PROJECT” ZOEZI LA KUTOKOMEZA MAZALIA YA MBU KATA ZA MANISPAA YA MJI BUKOBA


HARAKATI ENDELEVU ZA KIKUNDI CHA “BUKOBA MPYA PROJECT”

ZOEZI LA KUTOKOMEZA MAZALIA YA MBU KATA ZA MANISPAA YA MJI BUKOBA

Ndugu Wadau,

“Bukoba Mpya Project” ni zao la harakati endelevu chini ya Bukoba Wadau Media katika kuchangia kuhamasisha Wanabukoba wa ndani na nje ya Tanzania kushiriki katika kuinua hali ya mji na maisha ya wakazi wa Bukoba.  Wanachama wa harakati hizi ni waamini wa itikadi ya UMOJA na MAENDELEO. Mpaka sasa jumla ya wanachama wasioupungua 50 kutoka ndani na nje ya Bukoba na Tanzania kwa ujumla wanashiriki harakati hizi.

Wakiongozwa na imani kwamba “maendeleo yanaletwa na mimi”, Wana Bukoba Mpya wamepanga kuanza jitihada ya kupambana na Malaria kwa kutokomeza mazalia ya mbu kwenye maeneo yote ya Manispaa ya Bukoba. Jitihada hii itatekelezwa kwa zoezi la kupulizia dawa za kuua mazalia ya mbu kwenye Kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba. Zoezi litaanzia na Kata za Greenbelt  (Kahororo,Buhembe, Kitendaguro ,Ijuganyundo,Nyanga,Kibeta na Nshambya) mara tu baada ya siku kuu kuisha kisha litaendelea kwenye kata zingine zote kadri ratiba itakavyotolewa.

Kila mmoja anayeguswa na athari za mbu na anavutiwa na jitihada hii anaalikwa kushiriki kwa njia moja au nyingine. Unaweza kufanya hivyo kwa:

·         Kuthibitisha kushiriki moja kwa moja kwenye zoezi tarehe na mahali litakapofanyika
·         Kwa kuhamasisha ndugu na jamaa zako wafike kushiriki (hii ni kwa walio mbali na nje ya Tanzania)
·         Kwa kuchangia pesa, madawa na vifaa vya zoezi (orodha ya vifaa na utaratibu utapatiwa)

Viongozi, Watendaji na Wananchi kwa ujumla waombwa kutoa ushirikiano na kushiriki kwa kadri wanavyoweza pale zoezi hili litakapofanyika katika maeneo yao.

Kwa mawasiliano na maelezo zaidi juu ya jinsi ya kushiriki wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:
Mob: 0784 505045 / 0768 397241 /0713 883020 /0754 505043.


Imetolewa na:
Kitengo cha Uhamasishaji Jamii
Bukoba Wadau Media


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.