ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 10, 2015

CCM YAMSIMAMISHA JAMES BWIRE KUWANIA NAFASI YA MEYA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya ya Nyamagana katika uchaguzi wa kumsaka diwani atakaye simama kwa tiketi ya chama hicho kuwania nafasi ya Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza uliofanyika leo jijini hapa.
Diwani wa Kata ya Nyamagana mjini akitoa shukurani zake mbele ya wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kuinyakuwa tiketi ya CCM kuwania nafasi ya unaibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire, akitoa shukurani kwa wajumbe mara baada ya kuitwaa tiketi ya kuwania U'Meya wa  Halamashauri ya Jiji la Mwanza kupitia CCM.


Kutoka kushoto ni Charles Nyamasiriri, Yahya Shalia ambaye ni mchumi CCM Wilaya ya Nyamagana na Kaimu Katibu wa UWT wilaya ya Nyamagana.
Sehemu ya wajumbe wa mkutano.
Kutoka kushoto wadau meza kuu Katibu msaidizi CCM (W) Iddi Mkowa, Katibu wa UVCCM Mkoa Philipo Elieza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na Katibu Mwenezi  Mustapha Banigwa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu akitoa maelekezo kwa wajumbe wa uchaguzi huo.
Pongezi.
Shangwe na pongezi.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya na Jimbo la Nyamagana LEO wamewachagua, Diwani wa Kata ya Mahina, James Bwire, kuwa mgombea nafasi ya Meya wa  Halamashauri ya Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bikhu Kotecha, kuwania nafasi ya Naibu Meya.

Bwire alichaguliwa kugombea nafasi ya Meya kwenye kikao cha madiwani wa chama hicho kilichoketi leo katika ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana na Kotecha kuwania nafasi ya Naibu Meya baada ya majina kurejeshwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa ili kumpata mshindi ambaye atachuana na wagombea wa nafasi hizo kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Msimamizi wa Uchaguzi huo, Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Idd Mkowa, kabla ya kutangaza matokeo hayo alisema kwamba wagombea watatu ambao ni madiwani, James Bwire (Mahina) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule ya Alliance ya jijini mwanza inayomiliki pia Kituo cha michezo cha Alliance, John Minja (Igogo) na Dismas Ritte (Mkolani) majina yao yaliteuliwa na Kamati kuu ya CCM taifa ili kufanya uchaguzi ndani ya Chama na kupata mshindi.

Mkowa alisema kuwa Kamati Kuu ya CCM taifa pia iliwateuwa madiwani wawili, Bikhu Kotecha (Nyamagana) na Edithy Mdogo (Nyegezi) kuwania nafasi ya Naibu Meya na Katibu wa madiwani wa Chama hicho waliteuliwa diwani Donatha Gapi (Mkuyuni) na Mahamod Jama (Mbugani) ili kumpata mmoja atakayekuwa Katibu kwenye vikao vya madiwani wa Chama hicho Jimbo la Nyamagana.
Katibu huyo msaidizi anayekayimu nafasi ya Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana  akitangaza matokeo hayo alisema kwamba nafasi ya Meya Diwani Bwire amepata kura15 na kuibuka mshindi dhidi ya wapizani wake, Minja aliyepata kura 4 na Ritte aliyeambulia kura moja ya kwake pekee,nafasi ya Naibu Meya, Diwani Kotecha ameibuka mshindi kwa kura 16 na mpinzani wake Mdogo akipata kura 4.

Mkowa alimtangaza Gapi kushinda nafasi ya Katibu wa Madiwani wa Chama hicho kwa kupata kura 11 dhidi ya Jama aliyepata kura 9, pia aliwapongeza wagombea na madiwani kwa kutumia demokrasia ya kuwachagua viongozi hao ili kuhakikisha wanashirikiana kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Nyamagana.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wajumbe wa mkutano wa baraza la madiwani wilaya ya Nyamagana katika uchaguzi uliofanyika leo jijini hapa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, aliwataka viongozi hao na madiwani kuweka pembeni tofauti zao na badala yake wajikite kuwatumikia wananchi kama walivyowaahidi wananchi wakati wa kampeni pia kuendana na kasi ya Rais Dk John Magufuli, kuhakikisha Halmashauri ya Jiji haipati hati Chafu na iweke mipango ya maendeleo.


Kwa upande wake Meya aliyemaliza muda wake ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) amewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na madiwani wenzake na kuwaomba ushirikiano ili kutekeleza mahitaji ya wananchi bila kuwabagua kwa namna yoyote ile zaidi ya kuwaunganisha katika jitihada za maendeleo katika Mitaa, Kata na Jimbo hilo.

Madiwani, James Bwire (kushoto) aliyechaguliwa kugombea nafasi ya Meya wa Jiji la Mwanza, Diwani Donatha Gapi (katikati) aliyechaguliwa kuwa Katibu wa Madiwani wa CCM na kulia ni Diwani, Bikhu Kotecha aliyechaguliwa kugombea nafasi ya Naibu Meya jana kwenyekikao cha madiwani wa chama hicho.
Kesho Ijumaa utakuwa uzinduzi wa baraza la madiwani wa Jiji hilo ambao kikao cha uzinduzi kitaanza majira ya saa 3.00 asubuhi kwa kuapishwa madiwani wote wa Kata 18 za Jiji hilo pamoja na madiwani wa Vitimaalum kutoka vyama vya CCM na CHADEMA waliochaguliwa kabla ya uchaguzi wa Meya na Naibu Meya ambapo vyama hivyo vitawashindanisha wagombea wake waliochaguliwa na vikao vya madiwani ndani ya vyama hivyo.

CCM inao madiwani walioshinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kutoka Kata 14 kati ya 18 na CHADEMA wakiwa na madiwani Kata 4 huku CCM ikipata madiwani wa Vitimaalum 5 na CHADEMA wakiwa na Vitimaalum 1 hivyo kwa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya CCM wakiwa na nafasi kubwa kutwa uongozi wa Jiji hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.