ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 13, 2015

WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI,WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70

Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani) .
Baadhi ya iongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.
Wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame .
Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.
Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha  mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.