ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 26, 2015

RATIBA YA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO NA MAZISHI YA KAMANDA MAWAZO.

Mahakama kuu Kanda ya Mwanza imeamuru mwili wa marehemu Alphonce Mawazo uagwe jijini Mwanza, hukumuimetoka hii leo majira ya saa 16:15.

KESI ya msingi imemelizika kwa Mahakama hiyo kupitia Jaji Lameck Mlacha kuamua kwamba; 

Agizo la polisi la kuzuia kuagwa Kamanda Mawazo limefutwa na Mahakama Kuu.

Wafiwa wameruhusiwa na Mahakama kumwaga Kamanda Mawazo kwa kujadiliana na polisi sehemu ya kuagia.

Polisi watoe ulinzi kama ilivyo wajibu wao.



Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo
Kesho Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo.
Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda.
Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho.
Makene Tumaini Afisa Habari Chadema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.