ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 20, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA, MABULA ATAKA UONGOZI KUSITISHA ZOEZI LA KUWAONDOA NA KUWAZUIA WAFANYABIASHARA JIJINI HUMO

Stanslaus Mabula 
DODOMA.


MBUNGE wa Jimbo la Myamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kusitisha tamko na zoezi la kuwaondoa na kufanya shughuli zao wafanyabiashara wa mbogambonga, matunda, majisafi, juisi na mamalishe jijini humo kwa madai kuwepo ugonjwa wa kipindupindu na badala yake kuwaelimisha kufuata kanuni bora za afya.



Mbunge Mabula amesema hayo akiwa Mjini Dodoma kwenye shughuli za Bunge zinazoendelea baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo waliompigia  simu  kumpatia taarifa ili awasaidie  juu ya tamko na zoezi linalofanywa na Halmashauri kupitia Idara ya Afya ya Jiji hilo kuwazuia kufanya biashara katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya Kata 18 kutokana na tishio la kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu  jambo ambalo wamedai linawaathili katika kujitafutia kipato.



Mabula akizungumza na Blog hii ameutaka uongozi wa Jiji hilo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya, kusitisha tamko na zuio hilo la na badala yake wawaelimishe kwanza wananchi kupitia Idara yake ya Afya kwa kuwaeleza wafanyabiashara wa mbogamboga, matunda, maji juisi na vyakula vingine kuepuka kupanga dhidhaa zao sehemu zilizo safi na mamalishe watoe huduma ya chakula katika mazingira bora na yaliyo safi kwa  kufuata kanuni bora za afya zilizopo.



“Wananchi hao wanatakiwa kupewa elimu na kuelimishwa juu ya madhala ya ugonjwa wa kipindupindu uliolikumba jiji letu kwa wiki tatu ambapo  taarifa zilieleza watu saba walipatwa na ugonjwa huo na walitibiwa na jana wameruhusiwa baada ya kuthibitika kuwa wamepona, jambo hili likifanyika kwa kuwaeleza wananchi kutaondosha dhana na madai ya kuonewa ikiwemo kuondolewa katika maeneo yao ya kufanyia shughuli zao za kujiingizia kipato,”alisema.



Mabula alieleza kwamba kufatia hali hiyo amewasiliana na Kaimu Mkurugenzi Mahinya  kusitisha zoezi haraka na badala yake kupitia Idara ya Afya kupita na kutangaza kwa wananchi kanuni bora za kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu kwa wananchi hao jinsi ya kuzifuata ikiwa ni kuuza matunda, mbogamboga, vyakula sehemu zilizo safi na wasipange kwenye majimaji na mazingira safi.



“Mamalishe ambao wanahangaika kujitafutia kipato waelimishwe kwani wamekopa fedha za mitaji na kuanzisha biashara zao ni vyema wakapewa elimu kuzifuata kanuni bora za usafi katika mazingira ya tishio la kipindupindu kwa kutengeneza chakula na kukiuza kwa wateja wao katika mazingira safi na salama ikiwemo kuhakikisha vyakula saa zote vinakuwa vya moto, kuwepo na jiko lenye sufuria la maji ya moto ambapo ndani yake kutawekwa sahani, vijiko na vikombe ambavyo mamalishe watavitumia kuwapatia wateja wao chakula na siyo kuwaeleza wasitishe na kuondoka kama ilivyotangazwa ,”alisema.



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi, Mahinya alieleza kuwa kutokana na kubainika kuwepo ugonjwa wa kipindupimdu na watu saba kugundulika kupata ugonjwa huo waliochukua hatua za kuwazuia wananchi hasa wafanyabiashara wa matunda, mbogamboga na vyakula kupanga bidhaa zao chini sehemu zenye majimaji, lakini pia kuwazuia mamalishe kuendelea kuuza chakula kwenye vibanda na masoko ya jioni yaliyo kwenye mazingira machafu.



“Tumezungumza na Mbunge Mabula baada ya kupigiwa simu na kupewa taarifa na wananchi kuwa uongozi wa Halmashauri umewazuia kufanya biashara, lakini nimemuelewesha na tumekubaliana kuwa tutatumia gari la matangazo kupita tena kuwaeleza wananchi jinsi ya kufuata kanuni bora za mamalishe kutoa huduma ya chakula kwa wateja ili kuepuka kuambukizwa ugonjwa wa kipimdupimdu na wauzaji wengine kufanya usafi na kuacha kupanda vyakula chini  kwenye majimaji,”alisema.



Mahinya amewataka wananchi kuzingatia taratibu na kanuni za afya ili kuepuka kupatwa na ugonjwa wa mlipuko pia wadumishe utamaduni wa kufanya usafi na utunzaji mazingira ili kuendelea kuliweka jiji katika taswila ma muonekano wa usafi badala ya kukimbilia kulalamikia Halmashauri inapochukua hatua za kusitishwa utolewawaji huduma kwenye mazingira hatarishi na yasiyo salama kwa wateja na watumiaji kwenye baadhi ya maeneo ya masoko na vibanda vinavyotumiwa na mamalishe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.