ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 25, 2015

KESI YA MAWAZO YAPIGWA DANADANA NI KESHO TENA.



Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza hii leo imeahirisha tena shauri la kesi kutaka kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita jijini Mwanza Alphonce Mawazo.
Leo kesi hiyo imesikilizwa na hatimaye imepigwa kalenda  ambapo Jaji anayesimamia kesi hiyo ameamuru pande zote mbili kukutana tena hadi hapo kesho saa 7 pengine sasa ikawa ni kwaajili ya Hukumu. 



KESI hiyo namba 11 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa jana alasiri, inaoimba Mahakama kuondoa amri ya Kamanda Mkumbo kuzuia kuaga mwili wa Mawazo; kutoa tamko kwamba zuio la Mkumbo ni batili na kinyume cha sheria na kumkataza Kamanda Mkumbo kujihusisha na shughuli za mazishi na kuaga mwili wa Mawazo.
Mbele ya Mahakama Kuu ya Kanda Hapa Mwanza ambapo umati mkubwa ulifurika kutaka kujua nini hatma ya kesi hiyo nao ulinzi ukiwa umeimarishwa Mwanasheria wa Chadema, John Mallya ambaye ni mmoja kati ya mawakili watatu wanaoweka utetezi kwa familia ya Marehemu amesema haya baada ya kutoka chumba cha mahakama...(KWA YALIYOJIRI BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Katika kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama unakuwepo mahakamani hapo jeshi la polisi limeonekana likifanya doria kila eneo la barabara zinazounga njia za kuelekea eneo la mashauri.
Kutoka nje ya uzio wa Mahakama Kuu Mwanza jengo hilo linapakana na kivuko cha Kamanga, abiria wanaosafiri kuelekea Sengerema, Geita, Kagera na maeneo kadha walipita eneo hilo wakiwa na mshangao juu ya umati uliofurika mahakamani hapo. Chadema

Mbunge wa Bunda Ester Bulaya ni mmoja kati ya viongozi waandamizi wa Chadema waliopo jijini Mwanza kwaajili ya shughuli za mazishi ya marehemu Mawazo ambapo pia wamejitokeza mahakamani hapo kutaka kujua mwenendo wa kesi hiyo.
Wengine ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Ukongo Mwita Waitara, Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko, John Eche kutoka Tarime vijijini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu.
Mwanza.
Kutokana na wingi wa wafuasi hao, polisi waliongezeka maradufu na kutanda katika viwanja vya mahakama huku polisi wenye silaha wakiwa katika magari kila kona ya Mahakama.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wengine wafuatiliaji wa kesi hiyo wakiwa kwa misururu wakitawanyika katika mitaa mbalimbali jijini hapa toka viwanja vya Mahaka Kuu.

Kaimu Katibu mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu akiwa na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho ameendelea kutoa rai kwa watanzania, viongozi, wanachama ndugu jamaa na marafiki wanaoendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo kuendelea kuidumisha amani iliyopo ili kuwa mfano kwa dunia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.