ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 7, 2015

NDASSA NA KATIBU WA CCM MKOA MTATURU, WAOMBA WANANCHI MAGU KUWACHAGUA WAGOMBEA WA CCM KUMALIZA TATIZO LA MAJI SAFI

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa (CCM) akihutubia mamia ya wananchi na kuwaomba wawachague wagombea wa CCM ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika jimbo jirani la Magu alipoalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani wa Kata tatu za Mjini uliofanyika katika uwanja wa sabasaba jana mjini humo. Picha Na Peter Fabian.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akihutubia mamia ya wananchi wa Magu mjini na kuwaomba kuwachagua wagombea wa Chama hicho kuanzia ngazi ya Rais, Ubunge na Udiwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani wa Kata tatu za mjini uliofanyika  jana kwenye uwanja wa sabasaba mjini humo. Picha Peter Fabian.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kulia) akimunadi kwa wananchi mgombea Udiwani Kata ya Magu mjini, Mashaka Charles (kushoto) akiomba wamchague Oktoba 25, uzinduzi huo uliofanyika katika Uwanja wa sabasaba mjini humo jana Picha Na Peter Fabian.

Na Peter Fabian, Magu

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Sumve Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza, Richard Ndassa (CCM) amewaomba wananchi wa Jimbo la Magu kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama hicho, Boneventura Kiswaga, ili kusaidiana kumaliza matatizo katika sekta za maji safi, elimu, afya, umeme  na kuboresha miundombinu ya barabara ambalo ni changamoto kubwa la jimbo hilo.

Ndassa akizungumza jana kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za Udiwani wa Kata tatu za Mjini Magu zilizofanyika katika uwanja wa sabasaba  mjini humo, aliwaomba mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano huo kutofanya makosa ya kuchagua wawakilishi wao kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.
 
Ndassa aliwambia wananchi hao kuwa kutokana na Jimbo hilo kupakana na Jimbo la Sumve na historia yake huko nyuma amelazimika kufika kuwaomba ili kumchagua Kiswaga na Madiwani wa CCM ili Halmashauri ya Magu iweze kusimamia Ilani ya uchaguzi kwa vitendo lakini pia kushirikiana na Halmashauri ya Kwimba kuhakikisha matatizo na changamoto zilizopo timamalizika.

“Tunalo tatizo la maji safi mkumchagua Kiswaga ni lahisi kushirikiana naye kupigania hoja hii ndani ya Bunge ili serikali iweze kukamilisha mradi mkubwa wa maji fasi kutoka chanzo cha Ziwa Victoria ambao tayari umetengewa Sh bilioni 4 na Wizara ya Maji na wakati wowote Mkandarasi ataanza kazi hiyo, pia kuboresha barabara ya kutoka Hungumalwa- kupitia Nyamilama-Ngudu kupitia Sumve hadi Magu mjini kwa kiwango cha lami,”alisema.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, aliwahasa wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kutokana na kuwa na Ilani ya uchaguzi yenye dira ya kuwatumikia kuwaletea maendeleo katika Sekta zote za kijamii na kiuchumi ili kuhakikisha maendeleo ya haraka yanawafikia wananchi hasa walio na kipato cha chini.

Mtaturu aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kutokubali kudanganywa na wagombea walioazimwa na vyama vya upinzani kugombea Ubunge na Udiwani kwa kuwa hawana maandalizi ya kuwatumikia kwa dhati bali wanataka kutumia mgongo wa wananchi kuwachagua kwa masilahi yao binafsi na matakwa ya waliowachawapeleka kwenye vyama hivyo kugombea.

“Mchagueni Dr. John Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano, mchagueni Kiswaga kuwa Mbunge wa Jimbo hili, lakni tunao wagombea Udiwani Mashaka Charles Kata ya Magu Mjini, Sambo Lupondije Kata ya Itumbili na Velina Emmanuel Kata ya Isandula na kata zingine wa CCM ili kazi ya kuwaletea maendeleo itekelezwe kwa vitendo kama ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoelekeza,”alisisitiza.

Naye mgombea Udiwani Kata ya Magu mjini, Charles,  kwa niaba ya wagombea udiwani wengine wa Chama hicho aliwahakikishia wananchi kero za majisafi na uboreshaji wa barabara za mjini na upatikanaji wa huduma Katika Hospitali ya Wilaya ya Magu zinaboreshwa kwa kuhakikisha watakapo mchagua anazipigania kwenye Vikao vya Baraza la Madiwani ikiwa ni fedha za kununulia dawa na ruzuku inayotolewa na serikali ifanye kazi iliyokusudiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.