ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 11, 2015

MAHAKAMANI KWA KUGHUSHI TOVUTI FEKI NA KUTUMIA MAJINA YA TAASISI NA WANASIASA.


By Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam.  Watu wawili, Patrick Natala na Maxmillian Msacky  wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 10  yakiwamo ya kughushi, kutengeneza tovuti feki na mifumo ya mtandao  kwa kutumia majina ya  Taasisi, viongozi na wanasiasa.
Akiwasomea hati ya mashtaka leo Wakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa akishirikiana na Wakili Mwandamizi Mkuu wa TCRA, Johannes Kalungura walidai kuwa washtakiwa hao walitengeneza tovuti feki kwa kutumia majina ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Foundation (Ikulu), TCRA Foundation,  Akiba Saccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania na  Wekeza Fund.
Mutakyawa amedai kuwa  washtakiwa hao wametengeneza tovuti hizo feki kati ya Januari na Aprili  2014 jijini Dar es Salaam  kinyume  na kifungu cha 122 (b) cha sheria ya Kielektoliniki na Mawasiliano ya Posta  namba 3 ya 2010.
Mbali na mashtaka hayo, Mshtakiwa Msacky yeye anadaiwa kuwa kati ya 2006 na 2024 kwa njia ya udanganyifu alighushi cheti cha Sekondari  namba 0421130 chenye indexi namba S 0260-0001.
Iliendelea kudaiwa kuwa  kati ya 2005 na 2014 mshtakiwa huyo alighushi cheti kingine cha Sekondari  namba 0217951 chenye indexi namba S 0310-0532,akionyesha ni halali na kwamba vimetolewa na Baraza la Mitihani  Tanzania wakati akijua kuwa ni uongo.
Washtakiwa hao wamekana mashtaka na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika  na washtakiwa kupelekwa rumande hadi Septemba 28, 2015 itakapotajwa.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzage amesema kati ya Aprili na Juni  katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 walipata malalamiko toka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa makampuni feki yaliyokuwa yakidai kuwa yanatoa mikopo kwa muda mfupi.
Nzage amedai kuwa wahusika hao walitumia majina ya wanasiasa na pia kujifanya ni viongozi na wamiliki wa taasisi hizo na kwamba makumpuni hayo yanaandaa  shughuli za kuchangisha fedha. 
CHANZO: MWANANCHI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.