ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 1, 2015

BREAKING NEWS:- DR SLAA ANAZUNGUMZA HIVI SASA NA WAANDISHI WA HABARI LIVE

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho.

Leo ameibuka na kusema ya moyoni kuwa amejivua uanachama rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama cha hicho na kuaachana kabisa na siasa kutokana na mambo yaliyokuwayakifanyika ndani ya chama chake hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.
Dr. Slaa LIVE na wanahabari sikiliza pia kupitia 93.7 jEMBe fM.

WILBLOD SLAA-  Niliahidi mwaka huu CHADEMA hatuchukui Makapi, lakini aona wote walikuja ni mizigo nawajua A mpaka Z.

Wacha nizungumze sasa ili siku moja nitakapokufa wajukuu zangu watakapochimba kabuli langu watakuwa mashahidi kwa kusema hakika . 


 "Ni vema ijulikane kuwa nilishiriki majadiliano ya awali juu ya ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA, ila siafiki ujio wake.

*Baada ya July 11 Lowassa alipokatwa, mshenga wake, Bishop Gwajima alianza kuwasiliana nasi CHADEMA juu ya uwezekano wa kuhama. 

*Wakati tunajadiliana, Lowassa hakuwa ameshaamua kuhama CCM. Haikuwa busara kujadili mtu ambaye hajatangaza kuhama CCM.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.



INAENDELEA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.