ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 31, 2015

WATEJA WA AIRTEL WAZAWADIWA MILIONI 25 KUPITIA PROMOSHENI YA JIONGEZE NA MSHIKO

Meneja Mauzo wa Airtel Kagera , Mohamed Kabeke (kushoto) akimkabithi pesa taslimu bwana Mwahamadi Katula (24) mfanyabiashara na mkazi wa mkoa wa Kagera , mara baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni 3 katika droo ya wiki ya tano ya promosheni ya Jiongeze na Mshiko inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa uhusiano na matukio, Bi Dangio Kaniki akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya sita ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician.(kulia) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam,.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuchezesha droo za kila wiki na kuwazawadia wateja wake jumla ya pesa taslimu shilingi milioni 4 kila wiki baada ya kuibuka washindi katika droo za wiki za promosheni hiyo.

Akiongea wakati wa kuchezesha droo ya wiki ya sita ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema “ Tangu tuanze promosheni hii mwenzi wa Julai mwaka huu tumeshuhudia wateja wengi wakijishindia mamilioni ya fedha kila wiki na leo tumechezesha droo ya wiki ya sita na kuweza kupata washindi wawili ambao nao wamejishindia pesa taslimu.

Akiwataja washindi hao Kaniki alisema” ninayo furaha kumtangaza Rajabu Mwanalipanga (19) Mwanafunzi na mkazi wa Dar es Salaam kuwa mshindi wa shilingi milioni 3 na mshindi wetu wa pili ni Bwana Frank Kapesa (22) mkulima na mkazi wa Mbeya amejishindia shilingi milioni 1.

Promosheni hii bado inaendelea tukiwa tumebakiwa na takribani wiki 10 Za kuchezesha droo. Mpaka sasa shilingi milioni 25,000 zimeshatolewa kwa washindi waliopatikana kutoka katika mikoa mbalimbali.

Washindi hao ni pamoja na John Luu na Josephat Mahinda wakazi wa Manyara, Mwahamadi Katula Mkazi wa Kagera, Daudi Aliki na Agrisius Kapinga wakazi wa Dar es saalam, Rogers Shangali Mkazi wa Tanga, Gabriel Ferdnandi mkazi wa Musoma Mara, Hamisi Rashid mkazi wa Tabore, Rashid Hassani Mkazi wa Mtwara na Plasis Gabriel mkazi wa Geita.

Ili kushiriki mteja anatakiwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

 “ Jiongeze na Mshiko” inamwezesha mteja kujiunga na kushiriki bure kwa kujibu maswali na kujishinda shilingi milioni 1 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia milioni 2. Na pia kumwezesha mteja kujishindia zawadi kubwa zaidi kwa kujiunga na ngazi ya Premium kwa kuchajiwa shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milion 3 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia shilingi milioni 50

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.