ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 15, 2015

TaSUBa WATAMBULISHA RASMI TAMASHA LA 34 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

DSC_0016
Mwenyekiti wa Kamati kuu wa tamasha la 34 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Bw. John Mponda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika ukumbi wa MAELEZO mapema leo 8.14.2015. Wengine ni Mwalimu Christa Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa Maonyesho (kulia) na kushoto ni Bw. Frank Sika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Majukwaa na Ufundi wa tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu (Picha zote na Andrew Chale wa modewjiblog

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
(TaSUBa)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU .TAMASHA LA 34 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO.
Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.

Lengo kuu la Tamasha kwa wakati huo ilikuwa ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, baada ya Tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa chuo uliamua tamasha hilo lifanyike kila mwaka kwa kushirikisha Vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana Uzoefu na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.

Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo mwaka huu litafanyika kwa mara ya 34 kuanzia tarehe 21-27 Septemba katika kumbi na viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe Tanzania.

Tamasha la mwaka huu linabeba Kauli mbiu isemayo SANAA NA UTAMADUNI KATIKA UCHAGUZI HURU NA WA AMANI’ Aidha kutakuwa na mada ndogondogo zitakazotolewa kupitia kongamano na warsha zitakazohusu Haki za binadamu, Rushwa na kupinga Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)

Tamasha la mwaka huu litahusisha Ngoma za Asili, Maigizo, Sarakasi, Mazingaombwe, Muziki wa kisasa na asili, Sanaa za Ufundi na bidhaa mbalimbali.

Hadi sasa jumla ya vikundi 48 kutoka ndani na nje ya Tanzania vimethibitisha kushiriki,ambapo vikundi 43 ni kutoka ndani ya Tanzania na vikundi 5 kutoka nchi za Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.

Hadi kufikia sasa hakuna mdhamini yoyote aliyejitokeza kudhamini Tamasha hili na hii imepelekea vikundi kujigharamia na TaSUBa kugharamia Uendeshaji,hivyo Taasisi inatoa wito kwa wadau mbalimbali wa sanaa,Makampuni,Taasisi za serikali na zisizo za serikali kujitokeza kudhamini tamasha hili muhimu kwa mustakabali wa sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

Kwa yeyote anayehitaji kuchangia tamasha hili anaombwa awasiliane na Kamati ya maandalizi kwa mawasiliano hapo chini.

Mtendaji Mkuu, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania, Simu.: 0255 023 2440149
Barua pepe: bagamoyofest@gmail.com, Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Namba za Simu: +255(0) 754 310 425, +255(0) 787 542 242 na +255(0) 655 840 405
ASANTENI.
___________
JOHN MPONDA
M/KITI WA TAMASHA
14/8/2015
DSC_0029
Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho wa TaSUBa, Mwalimu Christa Kombo akifafanua jambo juu ya tamasha hilo kwa mwaka huu litakavyokuwa huku mambo mbalimbali yakiwa yamezingatiwa ikiwemo ubora wa vikundi na wasanii kutoka ndani na nje. Ambapo pia aliweza kufafanua juu ya maadili ya Sanaa katika tasnia ya burudani kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani). anayemfuatia ni Mwenyekiti Kamati Kuu ya Tamasha hilo la 34, Bw. John Mponda.
DSC_0040
Mwenyekiti wa Kamati ya Majukwaa na Ufundi wa TaSUBa, Frank Sanga akielezea idadi ya vikundi vitakavyoshiriki na namna TaSUBa ilivyojipanga katika kuboresha utamaduni kupitia tamasha hilo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.