ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 11, 2015

TOP 5 YAZUA VURUGU JIONI HII DODOMA, KUNDI LA LOWASSA HALIJAKUBALIANA NA MATOKEO.

VURUGU zimezuka mchana wa leo zilizodumu hadi majira ya alasili wakati kiza kikiingia wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea na mkutano wake.

Kutangazwa kwa majina matano na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa (CC-NEC) ya chama hicho jana usiku, kumeibua mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo, ambapo watatu wa wajumbe 32 wa kamati hiyo waliibuka wazi na kupinga uteuzi wa majina hayo mbele ya vyombo vya habari. 

 Baadhi ya Wanachama kwa idadi kubwa wameonekana waziwazi wakiandamana kuishinikiza Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM kulirudisha jina la mgombea wao Mhe. Lowassa.

 ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJILI.
Barabara kuu iendayo jengo kuu la Chama cha Mapinduzi mkoani (CCM) Dodoma, (Nyerere road) imegeuka kuwa ukumbi wa mkutano kwa umati wa watu kufurika.

Alasiri hii halmashauri kuu ya chama hicho ilifaanya kikao chake kupata majina matatu, halafu baadae leo jioni mkutano mkuu wa chama hicho unatarajiwa kukaa kupigia kura jina moja kati ya hayo matatu.

Yule atakayeibuka mshindi kati ya watatu hao ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ulinzi umeimarishwa.
Kutoka juu, taswira ya eneo la viwanja vya ukumbi wa mkutano sanjari na maeneo jirani.
Polisi wakiendelea kuwanasa wanaosadikika kufanya maandamano ambayo yanaashiria vurugu.
Wanachama wa chama hicho wametapakaa kila kona.
Mpasuko huu unaonekana kuwa mwanzo wa kutimia kwa utabiri wa wachambuzi mbalimbali ambao walionya mchakato huu unahatarisha uhai wa chama kikongwe nchini Tanzania.

Majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ni Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria) January Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Balozi Amina Salum Ali (Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani)

Kufikia Jumapili, tarehe 12. Julai, Watanzania watakuwa wamejua ni nani atakayekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM kwa uchaguzi mkuu ujao.

PICHA NA MWANDISHI WA Gsengo blog ZEPHANIA MANDIA: DODOMA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.