Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya
CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Katikati ni
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti Visiwani na
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya
Kikwete akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika
ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto)
akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia
katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama
hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi
wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto)
akipongezwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia
katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama
hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi
wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) (NEC) wakimpongeza Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia),
baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi
mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC, katika
ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe na Waziri wa Katiba na
Sheria, Dk. Asha Rose Migiro wakipongezana baada ya kuteuliwa kuingia katika
tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho,
kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
(kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membebaada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika
uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
jana.
KATIKA PICHA MAPOKEZI YA MWILI WA BALOZI DR KAMALA
-
Ni Simanzi kubwa mapokezi ya Mwili wa Balozi Kamala
Jeneza lenye Mwili wa mpendwa wetu
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Erasto Siima amewaongoza wananchi katika...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.