ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 27, 2015

JESHI LINAWASAKA WATU WAWILI WALIOHUSIKA MAUAJI KAHAMA

KAHAMA
JESHI la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawatafuta watu wawili ambao wamehusika katika matukio mawili tofauti  ya mauwaji ambayo yametokea  wilayani humo wiki iliyopita ili waweze kufikishwa mahakamani.

Akizungumuza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi  mkoani  Shinyanga Justus Kamugisha mkuu wa upelelezi kituo cha Polisi wilayani Kahama George  Bagyemu amesema jeshi linamtafuta Ntaki Mheziwa  mkazi wa mtaa  wa Ilindi anayedaiwa kumuuwa mke wake Mwajuma Mganda kutokana na ugomvi wa mali.

MSIKILIZE KAMANDA George


Aidha jeshi hilo linamtafuta  pia kijana mmoja  ambaye hajatambulika mara moja ambaye alimuuwa mwendesha pikipiki wiki iliyopita katika barabara itokayo Kahama kuelekea  Kakola halmashauri ya Msalala na kutokomea kusikojulikana akiwa kwenye harakati za kupora pikipiki hiyo.

MSIKILIZE TENA KAMANDA George


Hata hivyo jeshi hilo linaendelea kuwahamasisha waendesha pikipiki ili kuhakikisha kuwa wale ambao wanawabeba abiria nyakati za usiku kuwa makini nao kwani hao ndio wamekuwa wakisababisha mauwaji kwa waendesha pikipiki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.