ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 3, 2015

AIRTEL YATANGAZA OFA KABAMBE 'NUNUA AIRTEL HOME Wi-Fi NA UPATE NYINGINE BURE.

Ofisa uhusiano na Matukio  wa Airtel, Bi Dangio Kaniki akionyesha kifaa cha HOME Wi-Fi wakati wa kutangaza ofa kabambe ya Sabasaba itakayo wawezesha watanzania kupata kifaa cha bure cha ziada pindi watapokinunua katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba. Pichani, Afisa Masoko wa Airtel ,Ndevonaeli Eliakimu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe katika viwanja vya Sabasaba itakayomwezesha mteja kununua kifaa cha HOME Wi-Fi, chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 32 kupata huduma ya internet kwa kutumia kifurushi kimoja kwa gharama nafuu zaidi na kuunganishwa kwenye kifurushi cha internet cha 40GB Bure.

 Ofa hiyo itamwezesha mteja kununua HOME Wi-Fi, kwa shilingi 195,000/- na kujipatia Home Wi-Fi ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha 40GB cha bure .

Ofa hii inapatikana kwenye banda la Airtel katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba kwa muda wa kipindi hiki cha maonyesho. Akiongea wakati wa kutangaza ofa hii Ofisa uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema " Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja wetu kwa kuwapatia ofa hii ya kifaa kitakachowawezesha kuunganishwa kwenye huduma ya internet kwani mahitaji ya huduma ya internet yanazidi kuongezeka kwa kasi. Airtel HOME WiFi inaweza kuunganisha vifaa zaidi ya 32 kwenye huduma ya intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada".

"Sambamba na hilo, Airtel HOME Wi-Fi vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G.

Kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intaneti kwa kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye kifaa hiki cha HOME Wi-Fi na kuwawezesha wote waliounganishwa na kifaa hicho kupata huduma ya intaneti popote walipo Tanzania na watatumia kifurushi kimoja walichonunua"

"Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kutembelea Banda letu na kujipatia Home Wi-Fi na kuungalisha kweny internet wakati wote". Aliongeza Kaniki

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.