ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 24, 2015

UMISETA JIJINI MWANZA.

HOTUBA YA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA WAKATI WA KUFUNGUA MASHINDANO YA NGAZI YA MKOA YA MICHEZO YA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NSUMBA SEKONDARI TAREHE 23 MEI, 2015

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni Afisaelimu wa Mkoa na Viongozi wenzako katika seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Nimeupokea mwaliko huu kwa furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya wanafunzi, Wanamichezo na Walimu wao.  Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza uongozi wa Nsumba na Jumuia yote kwa maandalizi mazuri ya Mazingira kwa ajili ya mashindano haya.  Ahsanteni sana.
Ndugu Viongozi na Wanamichezo:
Leo tukumbushane umuhimu wa Michezo kwa Taifa na kwa mwanamichezo, mashindano haya ni nyenzo mojawapo ya kujenga Umoja wa Kitaifa na hivyo kufanya maelewano na mshikamano kwa Watanzania.  Michezo ni Burudani lakini kwa sasa kutokanana mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa vijana wetu, kukuza Biashara  na kujenga jamii bora yenye maelewano.  Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na Marekani, lakini nchi zingine za Afrika za Mataifa kama Nigeria, Togo, Ivory Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza  kiuchumi na kijamii.
Natambua kwamba ninyi ni Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo ni Michezo ili michezo iendelee kukua nchini, ni lazima ukuzaji wa vipaji vya michezo uanzie shuleni, ndiyo maana michezo ni sehemu ya Mtaala wa masomoyenu, kama ambavyo tunawataka mfanye bidii katika masomoyenu, fanye bidii pia na kukuza vipaji vyenu katika michezo kwa kushiriki kikamilifu kuonesha ubunifu.
Ndugu Wanamichezo,
Wanamichezo bora, ni Watu wasikivu, wenye nidhamu na watiifu.  Ninyi vijana ambao ndio viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana kujijengea nidhamu na maadili yahali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha ya ushindani yatakayokuwa  yanawakabili.  Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri unaofuata taratibu zote za kazi kwa wakati.  Hii ndiyo njia ya uhakikika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata mafanikio.
Aidha, kwa njia ya Michezo, nidhamu shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri pia katika matokeo  mazuri kwenye Taaluma.  Matarajio ni kuwa, wanafunzi watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na walimu wao na wale wote wanaopata Burudani ya Michezo.  Ama tunatarajia kuwa wataendelea kuwa watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.
Ndugu Wanamichezo,
Nitumie fursa hiipia kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke  kuwa furaha yenu itandelea  kudumu kama mtatambuakuwa kuna mpinzani mkubwa kati yetu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.  Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya Adui huyu.  Ni wajibu wangu kama Kiongozi na Mlezi wenu kuwakumbusha juu yahatari inayowakabili msipokuchua tahadhari ya kutosha.  Kumbukeni UKIMWI bado unaenea kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko rika lolote jingine.  Niwakumbushe kwamba upingine kwa nguvu zote   Ugonjwa huu.  Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na familia zenu.  Kwenu ninyi, njia bora pekee ni kusubiri hadi wakati muafaka wa ndoa.  Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.
Ndugu Wanamichezo,
Nimeelezwa kuwa baada ya Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na kuunda timu moja ya Kanda.  Ni muhimu timu zetu zijipange kushiriki vizurina kutuletea ushindi wa kishindo.  Aidha  timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki kama washidani na si wasindikizaji. Kushiriki kwenu kunatujengea heshima  katika kujenga upeo wa akili za vijana wetu na kujenga mahusiano mazuri ya kikanda.  Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine kushiriki kwa kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.
Ndugu Wana Michezo,
Nimalizie hotuba yangu kwa kuwatakia kila la kheri kwa kipindi chote cha mashindano, aidha msisite kuwasilianana ofisi yangu pale mtakapoonakuna ulazima wa kufanya hivyo kwa  ushauri na maelekezo kwa ajili ya kuboresha michezo hii.

Michezo hoyeeeeee!!!!


Asanteni kwa kunisikiliza

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.