ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 29, 2015

SKYLIGHT BAND NDIO HABARI YA MUJINI KWA SASA, KARIBUNI KIWANJA KIPYA CHA LUKAS PUB TUSEBENEKE LEO.

Skylight Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane Ijumaa hii ndani ya kiota cha Lukas Pub Masaki jijini Dar kwa kuburudika na band hii
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka kwenye stageni na moja ya nyimbo zao.
Joniko Flower naye katika muziki wa live hashikiki kwa sauti,viuno mpaka pumzi ni hatareeeee
KUNAKO Nigeria Flavour….. Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Watu navipaji vyao sasa team sky light band ikiongozwa na Ashura Kitenge katika miondoko ya zouk huku akisindikizwa na waimbaji wenzake katikaka,Sony Masamba pamoja na AK 47 meneja wa sky light band
sakata lumba na sky light band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba mmoja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi
Sugua sugua mpaka utakate ni nomaaaama saaanaa karibu leo kuna mambo mazuri ndani ya Skylight Band.
Skylight Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane Ijumaa hii ndani ya kiota cha Lukas pub Masaki jijini Dar kwa kuburudika na band hii
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kubwa mbele ya mashabiki wake huku akiwa na wasanii wenzake upande wa kushoto ni Sony Masamba na upande wa kulia ni sam mapenzikatika kiota cha Lukas, Masaki jijini Dar
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebenekaIjumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
kwaraha zao huku wakiwa wanafuatisha styl za bendi yao pendwa mashabiki walionekana na nyuso za furaha katika mstari mmoja tayari kwa kuyarudi.
Waimbaji wa Skylight Band wakizirudi sebene zilizokuwa zikiimbwa na Joniko Flower.
Sam Mapenzi pamoja(Kushoto) na Ashura Kitenge wakiimba kwafuraha huku wakiwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live na mwimbaji mwenzake Sony Masamba wakiwa wanaendelea kutoa burudani murwa kwa mashabiki wao.
Mbwembwe dizaini.
Ilikuwa noma sana jumamosi hii maana ilikuwa ni kubeneka mpaka kunakucha.
katika ubora wake Sony Masamba akiwa anaonyesha namna ya kucheza styl mpya na Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower.
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Lukas pub
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akiimba kwenye stage huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 wa kwanza kulia pamoja na Sony Masamba.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Ashura Kitenge.
baada ya kuonekana kukunwa na burudani inayotolewa na band ya sky light mashabiki wakaanza kulisakata.
wajanja wote tunakutana skylight band kila weekend kutupa shida chini na kuweka mikono juu huku viuno tukiwa hatuvisahahu kuvino sasa.
Mmoja wa mashabiki wa Bendi ya Skylight akichukua kumbukumbu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.