ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 9, 2015

TUNAWEZA BAND YAPIGWA TAFU NA AIRTEL.

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam , ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. 
Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanamuziki wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, kabla ya kukabidhi mkataba wa udhamini katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam, ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Anayeshuhudia (kulia) ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam, ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (wa pili kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.  

Waendeleza vipaji vya Walemavu hapa nchini • “Tunaweza Band” wawezeshwa kurekodi nyimbo zao mpya.

 KATIKA kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kutoa msaada kwa walemavu kupitia kikundi cha walemavu kijulikanacho kwa jina la “Tunaweza Band”, kwa kuwawezesha kulipia gharama za kurekodi nyimbo zao mpya. 

Makabidhiano ya mkataba huo kati ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na Ontime Production yalifanyika katika ofisi za Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar Es Salaam. 

 Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia kuifanya kulingana na msimamo wa kampuni hiyo wa kuwa karibu na jamiii inayowazunguka. “Msaada huu ni sehemu ya azimio tuliloweka la kuwekeza katika jamii yetu inayotuzunguka. 

Watu wanaoishi na ulemavu husahaulika katika jamii na hawapati haki zote zinazostahili kwa binadamu. Haki za binadamu ni sawa kwa watu wote bila kujali ulemavu wao. Kukosa uwezo wa kujihudumia mwenyewe, huleta mateso kwa binadamu yeyote yule. 

Tunafurahi kuwasaidia wenzetu katika jamii hii kwa kuwapa uwezo wa kujiongezea kipato kutokana na vipaji walivyonavyo.

 Naye Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka alisema kuwa amefurahishwa na moyo wa kampuni ya Airtel kwa kujali walemavu hapa nchini kwani wao si wa kwanza kupata msaada huu kutoka Airtel. 

“Nimefurahishwa sana na kitendo cha Airtel kujali walemavu hapa nchini na kwa kutusiadia kuongeza vipaji vyetu na vile vile kutuwezesha kuongeza kipato chetu kwani baada ya hapa tunauhakika wa kupata mikataba ya kurekodi nyimbo zetu nyingine nyingi tu ambazo tunazo.

Kwa niaba ya wenzangu wa kikundi cha Tunaweza, napenda kuwashukuru Airtel kwa moyo wao wa kujali watu walio katika mazingira magumu, hasa sisi walemavu. Msaada huu utatuwezesha na sisi kushirIki katika shughuli mbalimbali katika jamii pamoja na kufikia malengo yetu tuliyonayo.

Mnamo mwezi mmoja uliopita Airtel imewawezesha walemavu wengine kumi na tano kuweza kupata mafunzo ya biashara, mtaji na vibanda vya kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.