ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 30, 2015

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA VIONGOZI VIJANA KUTOKA AFRIKA NA CHINA.

Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alipowasili katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre)  uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China wenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) (Katikati) akisimama kwa ajili ya wimbo wa taifa kabla ya kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China jijini Arusha wenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alipowasili katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre)  uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China wenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) akihutubia mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha wakati wa kuufungua ramsi mkutano huo wenye lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo ya Afrika na China.

Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) akipeana mkono na Waziri wa mambo ya kimataifa wa China kutoka chama cha kikomunisti cha watu wa China(CPC)Mhe. Wang Jiarui mara baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) akionyesha  zawadi aliyokabidhiwa na Rais wa Youth Pan-African Union Bi. Francine Mayumba mara baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha.
Rais wa Youth Pan-African Union Bi. Francine Mayumba akimkabidhi zawadi  Waziri wa mambo ya kimataifa wa China kutoka chama cha kikomunisti cha watu wa China(CPC)Mhe. Wang Jiarui wakati wa kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha
Rais wa Youth Pan-African Union Bi. Francine Mayumba akimkabidhi zawadi  Waziri wa mambo ya kimataifa wa China kutoka chama cha kikomunisti cha watu wa China(CPC)Mhe. Wang Jiarui wakati wa kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka China mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa 3 wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China katika ukumbi wa (Tanzania Convention Centre) uliopo ndani ya hoteli ya kitalii ya Ngurdoto Mt. Lodge jijini Arusha.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
29/Machi/2015 Ngurdoto Mountain Lodge-Arusha, Rais wa Zimbambwe Mhe. Robert Mugabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amefungua rasmi mkutano wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unaofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ngurudoto Mt. Lodge.

Mkutano huu ambao  umeandaliwa rasmi na Umoja wa vijana CCM kwa kushirikiana na Chama cha kikomunisti cha watu wa China(CPC) umekua na lengo la kuhamasisha ushirikiano na kujenga uhusiano mwema kwa ajili ya kukuza uchumi kati ya Afrika na China.

Mapema jioni ya jana Rais Mugabe aliwasili jijini Arusha na kulakiwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Gharib Bilal ambaye aliambatana na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Stephen Masele.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Rais Mugabe ambaye wakati  wa mkutano alipewa majina mbalimbali kama “Mtoto wa kweli wa Afrika”  na “Kiongozi asiyetetereka” alisema anashukuru na pia anafurahia kualikwa kwenye mkutano wa viongozi vijana kama huu licha ya kwamba yeye ni mzee wa miaka 91. Alisema licha ya uzee wake akili na mawazo yake bado ni machanga kama walivyo vijana wenyewe na kuwapongeza kuwa wamefanya kitu sahihi.

“Katika ujana tunapambanua mapito yetu na katika uzee tunatengeneza  yajayo”. Mkutano kama huu ni njia mojawapo ya kuwa na ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya vizazi na vizazi na kuwafanya vijana kutengeneza kesho iliyo na matumaini... “Siwezi kukataa mwaliko wa kuja nchi kama ya Tanzania kwa kua tumekua bega kwa bega katika vita ya kupigania ukombozi na hapa ndipo mipango yote ya kupigania uhuru ilipo zaliwa”

Mkutano huo ambao ulianza mapema asubuhi ya tarehe 28 Machi 2015  mazungumzo yalianza kutoka kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali za Afrika ambao walizungumzia mambo mbalimbali muhimu  ya kimaendeleo, ushirikiano na urafiki kati ya China na Afrika.

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe ambaye nae alipata muda wa kuzungumza alianza kwa kuwakaribisha wageni wote nchini na kuongelea kile alichokiita “The Syndrome”(Uhusiano unaofanana) kati ya Afrika na China.  Mheshimiwa Membe alisema anafurahia uhusiano mzuri ulipo kati ya Afrika na China huku akiitaja nchi ya Tanzania kama mfaidika mkuu wa uhusiano huo.

Tanzania ina kila sababu ya kuishukuru nchi ya China kwa kuwa uhusiano wao na wetu ni wa kudumu na wameonyesha mapenzi ya dhati kwa waafrika ya kutaka kutusaidia alisema Membe.

“Angalia mfano wa reli ya Tazara ,uwanja wetu wa Taifa na Jengo la umoja wa Afrika (AU) ni baadhi ya maeneo na majengo ambayo wachina wametujengea bure bila kudai chochote” aliongeza Waziri Membe.

Hata hivyo Waziri huyo wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alisema anatarajia kuwa kupitia mkutano huu vijana wataweza kujifunza na kujadili njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana. “Ningependa wajadili kuhusu njia gani ya kuongeza ajira nchini kwa mfano kama ni biashara au uwekezaji basi waongelee kuhusu biashara zenye kuajiri vijana wengi kama viwanda vya nguo, cement au vile vya kusindika ili  kuweza kuwafaidisha watanzania walio wengi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.