ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 27, 2015

MTATURU AWASHUKIA VIONGOZI WA CCM NA WATENDAJI WA SERIKALI . MTATURU AWASHUKIA VIONGOZI WA CCM NA WATENDAJI WA SERIKALI.

Miraji Mtaturu.
NA PETER FABIAN, SENGEREMA.
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wametakiwa kuacha ubinafsi, rushwa na makundi, ndani ya Chama ili wananchi waendelee kukiamini na kukichagua tena kushika dola.

Pia wametakiwa kuacha kuwania nafasi za uwakilishi wa wananchi wakiwa tayari ni viongozi wa Chama na kama watafanya hivyo  ni vyema wakajiuzuru nyadhifa zao kwanza ili kupicha wengine kuchukua kutokana na wao kupenda kura mkate mwingine.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu wakati akizungumza na Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Sengerema, jana wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo ambayo pamoja na kujitambulisha, alikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Mtaturu amewaonya pia watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu na waliogeukia siasa na kuacha wajibu wao wa kutumikia wananchi, ole wao, Chama hakitawavumilia waendelee kukichafua. “Chama hiki tunakiua wenyewe kwa sababu ya ubinafsi wetu viongozi, unafiki, migawanyiko ya makundi na kundekeza rushwa hasa wakati kama huu wa uchaguzi, sasa iandaeni mioyo yenu kwanza muifanyie matengenezo na kaucha mambo hayo, Chama kwanza mtu baadaye,” alisema Katibu huyo.

Mtaturu alisema, watendaji wa serikali wanaokihujumu Chama wakidhani kitashindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, wanaota ndoto za mcha kweupe. CCM ni Chama cha mfano barani Afrika, watanzania wengi wenye mapenzi na uchungu na nchi hii, hawana mpango na vyama vinavyotaka kuvuruga amani.

Alisema CCM kitaendelea kutawala iwapo viongozi na watendaji watatumikia wananchi waliowapa dhamana na siyo kuangalia masilahi yao binafisi na kuendekeza rushwa na kujali matumbo yao.

“Nimeambiwa hapa kuna mtumishi wa maji anakata maji kwa maksudi na kupeleka mgao katika eneo jingine kabla ya muda uliowekwa, akipewa rushwa ndiyo anatoa maji na kuacha mgao uendelee, ole wake,” alionya na kumuagiza Mkuu wa wilaya hiyo Zainabu Telaki amshughulikie na ikibidi ang’olewe wilayani humo kwani ni adui wa CCM na wananchi wote.

Katibu huyo aliwataka viongozi hao na watendaji wa serikali wajitambue na kuthamini dhamana waliyopewa na umma, watumie nyadhifa zao kuondoa kero na migigoro ya wananchi huku wakikubali kukosolewa, kushauriwa na wasiwe miungu watu katika ofisi zao kwani CCM hutafuta kura na kutukanwa wao wakila raha tu.

Awali mkuu wa wilaya hiyo, Telaki akitoa taarifa ya mradi wa maji mjini hapa alisema  ameiagiza wagawa maji waweke maji katika vioski vipya 20 kwa kutumia gari la boza ili wananchi wapate huduma na kuonya kuwa atapambana na watumishi wabovu akiwemo anayedaiwa kutoa maji kwa rushwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.