ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 4, 2015

MAAFA MAKUBWA MKOANI SHINYANGA, WATU 35 WAFARIKI DUNIA KUFUATIA MVUA KUBWA KUNYESHA USIKU WA KUAMKIA LEO

Habari kutoka mkoani Shinyanga zinasema kuwa, zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 55 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. 

Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa. 

Mheshimiwa Mpesya amesema mpaka sasa hivi wamefanikiwa kupata miili ya watu 35 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu. 

Mkuu huyo wa Wilaya amesema nyumba nyingi zimeanguka na zoezi la kutafuta watu waliojeruhiwa au kupoteza maisha bado linaendelea kwa kasi. 

Tutawaletea taarifa zaidi hapo baadaye.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.