ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 9, 2015

KAYA ELFU 20 MIKOA YA KANDA YA ZIWA KUFUNGIWA UMEME WA SOLA ILI KUSAIDIA MAENDELEO KWA WANANCHI

 
Mgeni rasmi mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, Mhandisi wa Maji na Umwagiliaji kutoka Sekretalieti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Aron Kolongwa (watatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi la Mobisol Kanda ya Ziwa.  

Mkurugenzi Mwenyeji na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Kampuni ya Mobisol Uk Ltd ya jijini Arusha, Livinus Manyanga, akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa ofisi za tawi lake eneo la Kanyama Kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
 NA PETER FABIAN, MAGU.

KAYA zaidi ya elfu 20 za wananchi wanaoishi katika Vijiji, Mitaa na Kata za Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamelengwa kufungiwa mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Sola) kwa gharama nafuu kutokana na kuwa pembezoni na kutofikiwa na umeme wa gridi ya Taifa wa Shirika la Umeme Tanesco hapa nchini. 

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mwenyeji na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Kampuni ya Mobisol Uk Ltd ya jijini Arusha, Livinus Manyanga, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa ofisi za tawi lake eneo la Kanyama Kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza. 

Manyanga kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi huo, alisema kuwa Kampuni ya Mobisol Uk Ltd ni ya nchini Ujerumani ilianza shughuli zake hapa nchini mkoani Arusha mwaka 2011na kujitanua zaidi katika Ukanda wa Mikoa ya Kaskazini ya Manyara, Kilmanjaro na Arusha na sasa imeingia Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 “ Lengo ni kupunguza umasikini wa upatikanaji wa nishati ya umeme hapa nchini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya nishati vijijini , kuangaza maisha ya jamii zetu na kufanya mazingira kuwa sehemu bora ya kuishi kutokana na kufungiwa mitambo ya Sola za majumbani ambazo ni endelevu na rafiki kwa mazingira,”alisema.
Mobisol.
Kutokana na utafiti uliofanywa na Kampuni yake mwaka 2012 hadi 2014 iligundua kuwepo hitaji kubwa la umeme wa Sola kwa ukanda wa ziwa ambapo Mobisol imekusudia kufunga mitambo ya nishati hiyo katika Kaya zaidi ya elfu 20 Kanda ya Ziwa huku Mkoa wa Mwanza pekee ikikusudiwa Kaya 6,270.
Wadau wa Mobisol
Takwimu zinaonyesha Wilaya ya Ilemela ina asilimia 14, Nyamagana asilimia 18 tu ya walio na huduma ya umeme wa gridi ya taifa huku wilaya zingine zote zikiwa na asilimia 2 hivyo kupitia umeme wa Sola utasaidia kupunguza uhaba wa nishati ya umeme katika maeneo mbalimbali ya wilaya hizo na mikoa ya Kanda ya Ziwa.  Mitambo ya Sola Energy ya Mobisol imekidhi vigezo vya ubora wa kimataifa na huuzwa kwa bei nafuu na kwa mkopo wenye liba ndogo kwa wateja wake wanaofika katika ofisi za tawi la Kampuni, pia ombi letu ni ushirikiano na wananchi na Serikali ya Mkoa wa Mwanza kutupatia eneo la wazi kuweza kutoa elimu ya mitambo yetu ili kuwashawishi wateja kabla ya kuwafungia.
Ujumbe madhubuti ulipenyezwa kupitia maigizo.
Mobisol mkombozi wa afya za wananchi mijini na vijijini, kwani badala ya kutumia koroboi ambayo uharibu afya na macho kuanzia sasa kupitia matumizi ya taa na majiko yanayotumia umeme wa nishati ya jua (sola) afya zitaimarika na kuwa salama.

Naye mgeni rasmi mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, Mhandisi wa Maji na Umwagiliaji kutoka Sekretalieti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Aron Kolongwa, alipongea ujio wa Kampuni hiyo mkoani humo na Kanda ya Ziwa na kuishukuru kwa kutoa mitambo mitano ya Sola ambapo itafungwa katika maeneo ya shughuli za utoaji huduma za kijamii. 

Kolongwa alisema kuwa kupatikana kwa wadau wa maendeleo wa nishati ya mumeme wa sola kutaongea kasi ya maendeleo katika maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati ya umeme wa gridi ya taifa na kusaidia wananchi kujikwamua na umasikini kwa kutumia umeme wa sola katika mwanga na biashara na kuimalisha ulinzi katika maeneo ya makazi yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.