ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 2, 2015

KAPTENI KOMBA AAGWA LEO JIJINI DAR KUZIKWA KESHO.

Mamia wamuaga marehemu John KombaRAIS Jakaya Kikwete leo amewaoongoza mamia ya waombolezaji waliofika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuuaga mwili wa mbunge wa Mbinga magharibi Kapt John Komba aliyefariki Jumamosi iliyopita njiani wakati akipelekwa Hospitali ya TMJ.
Mwili wake ulipokelewa kwa heshima huku ukiwa umebebwa na Askari wa bunge.
Ndugu jamaa na marafiki walikuwa katika huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao huyo. Wapo waliopoteza fahamu kutokana na kushindwa kuamini tukio hilo.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa wamehudhuria akiwemo Mhe. Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na wengine wengi.
Wasanii walimuenzi marehemu Komba kwa kuimba nyimbo za maombolezi ambazo aliziimba enzi za uhai wake wakati wa msiba wa Baba wa Taifa, Hayati J.K.Nyerere mwaka 1998.
Katika salamu zake kwa niaba ya kambi Rasmi ya upinzani Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh.Joshua Nasari ametoa pole kwa familia ya marehemu na taifa.
Mh Nasari alisema kwamba kambi rasmi ya upinzani imeguswa na kifo cha mwanasiasa mwenzao kwani kila mmoja atarejea na huko ndiko kila mmoja atakwenda.
Pia Mh Nasari amesema katika kipindi hiki kigumu ni vyema kila mmoja akasali na kuomba muda wote ili kujiwekea mazingira mazuri huko aendako.

Moja ya mambo yaliyohuzunisha ni taarifa aliyoitoa Mh Cyril Chami mbunge wa Moshi vijijini ambapo alisema siku ya Jumamosi ambayo alifariki Mh Komba, aliwasiliana nae kwa simu mda mchache kabla hajazidiwa ambapo Mh Chami alikuwa njiani kwenda kumuona.
Anasema alipofika nyumbani akaambiwa Mh Komba amezidiwa hivyo wamempeleka Hospitali ya TMJ.
Mh Chami alienda TMJ hata hivyo alipofika getini alikutana na gari la kubeba wagonjwa likiupeleka mwili wa marehemu Komba chumba cha kuhifadhi maiti.
Kweli binadamu inabidi kuwa tayari muda wote kwani hatujui saa wala dakika ya kurudi kwa muumba wetu. 
Tufanye mambo mema ya kumpendeza Mwenyezi Mungu kwani dunia ni mapito tu.
Tumuombee safari njema mwenzetu kwani sote tuko njia moja. Amen.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.