ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 29, 2015

FULL TIME: TAIFA STARS 1 vs 1 MALAWI, MBWAN ALLY SAMATTA AIOKOA STARS CCM KIRUMBA MWANZA

Pongezi kwa Samatta Ally Mbwana.
SIKILIZA TAARIFA TOKA UWANJANI

Taswira Viongozi na Timu zote mbili wakati wa dakika chache kumbuka Kiongozi wa mpira Aliyekuwayetangulia mbele ya haki kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Star Sylvester Marsh aliyefariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Mjini hapa hapa Mwanza.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika Mpambano huo wa Taifa Stars na Malawi CCM Kirumba  Jijini Mwanza leo Jumapili tarehe 28.03.2015
Timu zikisalimiana.
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza.
Waamuzi wa Mtanage.
Kikosi cha Malawi.
Tayari kwa mpambano kuanza..
Shilingi kutafuta uelekeo.
Picha ya Pamoja.
Bao 1-0 dakika ya tatu tu Malawi walipata bao kupitia kwa Esau Kanyenda baada ya mapeki wa Stars kujichanganya.
Wachezaji wa Malawi wakipongezana baada ya kupata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Esau Kanyenda kwa kufanya 1-0.
Mchezaji wa Malawi akimiliki mpira.
Hatari!
Taifa Stars 0-1 Malawi dakika ya 3 mapema Malawi walishachafua ubao.
Kipa wa Malawi akiondosha mpira langoni mwake.
Pisha!
Fundi!
Kipa wa Malawi akiondosha mpira kwa kuupangua kutoka eneo la hatari
Mashabiki waliingia kwa wingi leo CCM Kirumba.
Mashabiki jukwaa kuu
Meza Kuu Rais wa Tff  Bw. Jamal Malinzi nae alikuwepo kushuhudia kipute!
Nyomi
Katikati ni Bw. Abdrazack kutoka Mjini Bukoba/Kasibante 88.5 FM Radio akitangaza live mpira huo kutoka CCM Kirumba Jijini Mwanza
Mashabiki waliingia kwa wingi
Mpaka mapumziko Stars ilikuwa nyuma ya 1-0
Waamuzi wakitoka kwenda kupumzika wakati wa mapumziko dakika chache
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Stars Mart Nooij akiteta jambo na Kiongozi wa soka wakati wa mapumziko baada ya dakika 45 kupita, wakiteta jinsi ya kupangua na kuweza kusawazisha na hatimae ushindi!! Kipindi cha pili tunafanyaje??? Ngassa aingie au??

Muuaji wa bao la Malawi Essau kanyenda wakati wa mapumziko
Yale yale Ngassa na wenzake wakitoka Uwanjani kwenda kujumuika na kusikia neno kutoka kwa kocha mkuu Mart Nooij nini kinafanyika kipindi cha pili.
Patashika kwenye lango la Malawi kipindi cha pili
Mbwana Ally Samatta akishangilia bao baada ya kuisawazishia bao Taifa Stars kwa kufanya 1-1 dakika ya 76 kipindi cha pili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo hii, Picha na Faustine Ruta
Asante baba!! Samatta akipongezwa
1-1
Samatta akipongezwa
Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars nao walimpongeza Samatta.
Wakishuhudia live Mtanange CCM Kirumba
Mtanange umemalizika dakika 90 kwa nguvu sawa 1-1

Waandishi wa Habari wakipata mahojiano moja kwa moja kutoka kwa Afisa habari wao Malawi akiwa sambamba na Baraka Kizuguto wa Tanzania kupitia Tff

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.