ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 19, 2015

MENGI YAIBULIWA LEO KATIKA MAFUNZO YA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA NA MAAMBUKIZI YA VVU KWA WAANDISHI WA HABARI NA WATOA HUDUMA MWANZA

Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Yassin Ally akiwasilisha maelezo kuhusu mradi wa mpya ujulikanao kwa kifupi SASA katika semina ya mafunzo ya kuzuia ukatili wa kijinsia na maambukizi ya VVU kwa waandishi wa habari na watoa huduma iliyoanza leo katika ukumbi wa mikutano Hillfront Hotel Igoma Mwanza. 
BAADHI ya Waandishi wa Habari na Watoa huduma mkoani Mwanza wamekutanishwa katika Mafunzo ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI.
Mafunzo hayo yanatolewa kipindi hiki ambapo Mikoa ya kanda ya Ziwa inatajwa kuongoza nchini kwa vitendo vya Ukatili hususani wa kijinsia. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)

Meneja wa mradi wa SASA wilayani Misungwi Bi.Juliana Myeya akiwasilisha maelezo kuhusu mradi, malengo, utafuti, changamoto  na jinsi utakavyofanya kazi katika awamu ya pili na ya tatu.   
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KIVULINI Gasper Mwanalyela (Wakili) akiwasilisha changamoto na ugumu wa upatikanaji wa haki kwa wanawake wanaotendewa Ukatili wa kijinsia kupitia sheria ya ndoa na sheria ya Ardhi.
Maimuna Kanyamala ni Muasisi wa Shirika la KIVULINI anabainisha hali ya kijinsia ilivyo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)

Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo.
Kwa upande wake mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Jonathan Shana ametumia ufunguzi wa mafunzo hayo kutoa salamu kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya Ukatili. (BOFYA PLAY MSIKILIZE)

Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo.
Mwandishi wa habari toka Sahara Media Maliganya Charahani akishiriki kutoa uzoefu wake kuhusiana changamoto mbalimbali alizozibaini wakati wa ukusanyaji taarifa za Ukatili wa kijinsia ambazo zimekuwa sugu katika jamii dhidi ya wanawake na watoto.
Suala la katiba iliyopendekezwa ikisubiri kupigiwa kura nalo halikusahaulika ambapo Serikali imeombwa kuharakisha zoezi la kuchapisha katiba iliyopendekezwa na kuisambaza mapema ili wananchi wapate muda wa kutosha kuipitia kabla ya kuipigia kura  ili kubaini kama kuna mapungufu hususani vipengele vilivoongezwa kumpa nafasi zaidi mwanamke. (BOFYA PLAY SIKILIZA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.