ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 4, 2015

BENKI YA I&M YAZINDUA HUDUMA YA KWANZA YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI YA MASAA 25 KATIKA JENGO LA VIVA TOUR,POSTA JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha  (kushoto) akiongea na wadau wa benki hiyo hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa tawi  na mfumo mpya wa kielektroniki uliovumbuliwa na Smart Banking Solutions Ltd ambapo mteja anaweza kuweka na kutoa pesa  sambamba na kupata huduma nyingine za kibenki kama kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mashine za kielektroniki masaa 24 ya siku.Hafla hiyo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja wa I&M wa tawi hilo Bi. Shabina Manji.
Baadhi ya wadau wa benki ya I&M na waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw. Anurag Doreha , hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la kielektroniki , ambapo wateja wake wataweza kuweka na kutoa pesa kwa kutumia ATMs sambamba na huduma ya kubadili fedha za kigeni kwa masaa 24. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi jipya la I&M, Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam. Benki hiyo imeungana na kampuni ya Smart Banking Solutions kuwaletea wateja wake huduma hii
Mkurugenzi Mkuu wa VIVA Tower Viral Manek, akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya I&M katika jengo hilo litakalotoa huduma masaa 24, kwa kuweka na kutoa fedha na kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mfumo mpya wa mashine za kieletroniki (ATMs). Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, Bw. Anurag Doreha, Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha (katikati) akifafanua jambo baada ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo kufanyika katika jengo la Viva Tower ambapo huduma za kuweka, kutoa na kubadilisha fedha za kigeni zitakua zikifanyika masaa 24 kutumia mashine za kielektroniki(ATMs) kulia ni Mkurugenzi mkuu wa VIVA Tower Viral Manek na kushoto ni Meneja Masoko wa Smart Banking Solutions Limited, Salil Abbas Sadik. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa VIVA Tower Viral Manek, akionesha kwa vitendo jinsi ya kuweka fedha katika moja ya mashine za kielektroniki ndani ya tawi jipya lililozinduliwa la benki ya I&M ikishirikiana na Smart Banking Solutions-Viva Tower-Posta jijini Dar es salaam ambapo mteja anaweza kuweka na kutoa fedha masaa 24 sambamba na kupata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mashine za kielektroniki(ATMs).
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya mashine inayotumika kubadili fedha za kigeni, baada ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo maalum kwa shughuli za kuweka na kutoa fedha kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki kupitia mashine za (ATMs). Hafla hiyo ilifanyika katika jengo la Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam ambapo benki hiyo imeshirikiana na kampuni ya Smart Banking Solutions Ltd.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha akionyesha mfano wa kutoa fedha katika moja ya mashine inayotumika kubadili fedha za kigeni. Mare baada ya kuzindua tawi na mfumo mpya ulioanzishwa na Smart Banking Solutions wa kuweka na kutoa fedha kupitia ATMs sambamba na kubadili fedha za kigeni ambapo mteja atapata huduma hii ndani ya masaa 24 ya siku. Hafla hiyo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar.
Meneja Masoko wa Smart Banking Solutions Limited  Bw. Salil Abbas Sadik akiwaeleza waandishi wa habari kwa undani jinsi mfumo huo  wa kielektroniki unavyofanya kazi ambapo mteja anaweza kuweka na kutoa fedha kupitia mashine za (ATMs) sambamba na kubadili fedha za kigeni masaa 24. Smart Banking solutions Ltd ndio waanzilishi wa teknolojia hiyo ambayo bado haijatumiwa na benki nyingine yeyote. Hafla hiyo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar.
Meneja Masoko wa Smart Solution limited, Salil Abbas Sadik. Akiongea  na wadau wa Benki ya I & M hawapo pichani , wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo lililo katika Jengo la Viva Tower ambapo huduma zitatolewa masaa 24, ikiwemo kutoa ,kuchukua na kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mashine za kisasa za kielektroniki za ATM, Uzinduzi huo ulifanyika katika jengo hilo la Viva Tower Jijini Dar es Salaam

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.