ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 25, 2015

NANI MKALI BUKOBA MOVIE HIYOO YAJA RAUNDI YA PILI. KUANZA JUMAPILI FEBRUARY 8, 2015

Mwandaaji wa Vipindi vya Nani mkali Bukoba Movies Tesso Boy(kushoto) akiwa na Mwimbaji wa nyimbo za asili Revina kasabila Nchini wakiingia katika Ukumbi wa Kiroyera Beach Jioni ya Leo Jumamosi 24, Januari 2015 Katika Maandalizi hayo ambayo yataanza mwezi ujao wa pili katika Siku ya Jumapili tarehe 8.

Vijana wakifurahia baada ya kukutana sehemu hiyo na kupongezana kwa kupeana heri ya Mwaka mpya 2015 na kujiandaa kwa mambo mapyaa ya mwaka huu.
Mwimbaji wa nyimbo za asili Revina kasabila(katikati) akiwa na Ndugu yake Bw.Brighton Kasabila (kulia) leo Jumamosi tayari kwa kuanza mashindano hayo ya Nani Mkali Bukoba ambayo Uwakutanisha Wasanii wa hapa Bukoba.Dada Revina Kasabila(kushoto) akiongea na Vijana/Wasanii ambao watachuana Vikali na Kupata Mkali wao kuanzia Mwezi Ujao siku ya jumapili tarehe 8. Nani Mkali ni Sehemu kubwa ya Vijana wa kuigiza ambapo uwakutanisha Watu wa kila rika bila kubagua sura umri wala kabila.Mkali wa Nymbo za asili Nchini Dada Revina Kasabila(kushoto) aliyetamba na Nyimbo kadhaa kama Katerero, Tembelea Kagera akiteta na Vijana waliokusanyika katika Ufukwe huo wa Kiroyera ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya Mtanange huo utakaokuja kwa kasi mwezi ujao na kwa aina yake.
Vijana wakifurahia baada ya kukutana sehemu hiyo na kupongezana kwa kupeana heri ya Mwaka mpya 2015 na kujiandaa kwa mambo mapyaa ya mwaka huu.

Mapema mwandaaji Tesso Boy akiongea na tandao huu amedai kuwa nafasi bado zipo hivyo anawaomba Vijana wajitolee wenye Vipaji ili waweze kushiriki kwani muda bado upo.  Kwani Wasanii wa kuigiza wanatakiwa kuwa 20 na Kundi la Kucheza(Dancers) wanatakiwa kuwa 10. Na aliongeza pia kuwa Mashindano ya Mwaka huu 2015 yatakuwa na mabadiliko makubwa na zawadi za Washindi zitaongezeka maradufu.

Mwandaaji Tesso Boy(kulia) akitokelezea kwenye picha na rafiki yake Ufukweni Ziwa Victoria.

Mwimbaji wa nyimbo za asili Revina kasabila Nchini.

Mweneja wa sasa wa Kiroyera TOURS Bukoba Bw. Aaron Kalikawe nae alikuwepo 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.