ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 30, 2015

MRBA YAZIBA NAFASI 4 ZA JUU ZILIZOKUWA WAZI NA KUUNDA UONGOZI WA MUDA

Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa mwanza (MRBA) kupitia kamati ya michezo mkoa wa Mwanza kimetangaza majina ya viongozi wa muda ambao utakuwa madarakani kwa muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe 01.02.2015.

Lengo kuu la kutangazwa viongozi hawa pamoja na kuziba nafasi za viongozi waliokuwepo awali, ni kuwataka viongozi hawa kufanya uchaguzi mkuu sambamba na kuzielekeza klabu mbalimbali kufanya uchaguzi wa viongozi katika klabu ili waweze kushiriki uchaguzi ngazi ya mkoa.

Viongozi hawa wanaziba nafasi za viongozi waliokuwepo awali ambao kwa sasa hawapo kutokana na sababu mbalimbali.

Uongozi wa awali ulikuwa ni kama ifuatavyo:

11.      Sadoti Mazigo (Mwenyekiti) – alihama mwanza.
22.      Adam Nyoni (Makamu Mwenyekiti) – alihama mwanza.
33.      Chikoko (Katibu Mkuu) – alihama mwanza.
44.      Victor Maleko – Katibu msaidizi
55.      Flora Kavavila – Mweka hazina (Alifariki)
66.      Amri Mohamed – Kamishna wa Makocha.
77.      Twalib Puzo – Kamishna wa Waamuzi.
88.      Diana Deodatus – Kamishna wa wanawake.
99.      Haidary Abdul – Kamishna wa ufundi na uendeshaji mashindano.
110.  Kizito Bahati – Kamishna wa watoto na maendeleo ya mashule.
111.  Vincent Shinda – Mchezaji mwakilishi.

Nafasi zilizozibwa ni wahusika ni wafuatao.
11.      Juvenile Kaiza ­– Kaimu Mwenyekiti. 
22.      Benson Nyasebwa – Kaimu Makamu Mwenyekiti.
33.      Shomali Almasi – Kaimu Katibu Mkuu.
44.      Vitalis Ndanu – Kaimu M/Hazina

Viongozi hawa watashirikiana na waliopo katika kuendeleza mpira wa kikapu mkoa wa mwanza.
Imetolewa na:

Kizito Sosho Bahati
Kaimu Katibu Mkuu
MRBA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.