ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 7, 2015

MKAZI WA DAR AIBUKA NA USHINDI MNONO KWENYE KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI

Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa Limo bajaj na fedha taslim Tsh 100,000/= katika Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA kushoto ni  msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Majjid , ambapo Godfrey Longino Mpiruka mkazi wa Dar ameibuka na ushindi mnono. Droo hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti-Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA. Kushoto ni  msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Majjid na kulia ni Meneja Vipoozeo na mwonekano, Baraka Mandara,  ambapo Bw.Godfrey Longino Mpiruka mkazi wa Bunyokwa, Segerea Dar es salaam ameibuka mshindi wa Limo Bajaj yenye uwezo wa kubeba watu 7 na fedha taslim Tsh. 100,000/=. Droo hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti-Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA
RE: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKAZI WA DAR AIBUKA NA USHINDI MNONO KWENYE KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI
7th Dec 2015, Dar-Es-Salaam
Mwaka 2015 umeanza vizuri kwa Bwana Godfrey Longino Mpiruka  baada ya kutangazwa mshindi wa nne wa bajaji mpya aina ya Limo sambamba na fedha taslim Tsh. 100,000/= zinazotolewa kila wiki katika kampeni  inayoendelea ya  “Tutoke na Serengeti” .

Godfrey mwenye umri wa miaka 47 na mkazi wa Bunyokwa Segerea-Dar es salaam ameibuka na ushindi huo mnono baada ya kuwashinda washiriki kutoka mikoa ya Moshi na Morogoro ambayo mpaka sasa  imeongoza kwa kutoa washindi mbalimbali katika kampeni hii ya miezi mitatu inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium lager kwa kushirikiana na BPESA.
“Wakati nashiriki katika kampeni hii, lengo langu lilikuwa ni kushinda shilingi 100,000/= bila kujua kwamba ushiriki wangu ungenipelekea kushinda pia Limo Bajaj mpya..ninashukuru sana Serengeti” alisema Bw.Godfrey kwa njia ya simu mara baada ya kuibuka mshindi wa nne wa Limo Bajaj. Godfrey aliongeza kwamba, Bajaji hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 7 ambayo imeigharimu SBL kiasi cha Tsh. 9,000,000/= itamsaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato katika maisha yake na pia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifedha ambazo amekua akikabiliana nazo.

Baadhi ya washindi waliofaidika na kampeni hii na kupata zawadi zao ni pamoja na: - Bi. Rukia Almasi ambaye ni mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda aliyeshinda bajaji ya kwanza, wakati  Peter Emmanuel, dereva wa  bodaboda aliibuka mshindi wa pili, na Isaack Edward Maro mwalimu wa shule ya awali kutoka mkoa wa Kilimanjaro aliibuka mshindi wa tatu. Kwa upande mwingine, Hassan Mfaume na Deogratias Masenga kwa pamoja walishinda safari ya siku mbili na wenza wao ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti National park na zaidi ya washindi saba walijinyakulia kitita cha shilingi  100,000/= kila mmoja zilizokuwa zikitolewa kila wiki baada ya droo.

Akiongea na waandishi wa habari Bw. Rugambo Rodney, Meneja wa bia chapa Serengeti Premium Lager alisema….“ Promosheni ya Tutoke na Serengeti bado inaendelea na kama ilivyo ada, SBL kwa kushirikiana na BPESA wanaendelea kuwazawadia wateja wao zawadi mbalimbali zikiwemo Limo Bajaj, safari za bure za kutembelea mbuga za wanyama, fedha za papo kwa hapo kiasi cha shilingi  100,000/= kila wiki, punguzo la bei la shilingi 300/= katika bei halisi ya bia aina ya Serengeti, pamoja na bia za bure ambazo zinatolewa nchi nzima.” Rodney aliendelea kueleza kuwa promosheni imeendelea kufanya vizuri tangu kuanza kwake kwa muda wa miezi miwili iliyopita na hivyo basi uongozi umeona ni vema kuongeza mwezi mmoja wa promosheni ili wateja waendelee kujinyakulia zawadi mbalimbali.

Promosheni hii ya nchi nzima ilizinduliwa na SBL pamoja na B-Pesa miezi miwili iliyopita ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake katika kila droo itakayokuwa ikifanywa kila wiki na SBL chini ya uangalizi wa bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.

Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja anatakiwa awe na umri wa zaidi ya miaka 18, na anunue bia ya Serengeti Premium Lager na kuangalia chini ya kizibo ambapo atakuta namba zinazotakiwa kutumwa  kwa njia ya SMS kwenda 15317. Kadiri mteja anavyoshiriki zaidi ndivyo anavyojiweka katika nafasi nzuri ya kushinda zaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.