ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 28, 2015

UKAWA WASIMAMISHA SHUGHULI ZA BUNGE HII LEO LAAHIRISHWA MPAKA KESHO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda akiahirisha shughuli za bunge leo asubuhi.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ameliahirisha Bunge hadi kesho baada ya kutokea mabishano kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mhe. James Mbatia akitaka kujua hatma ya Vurugu zilizotokea jana mara baada ya kukamatwa kwa wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali. 

Mbatia aliomba suala hilo lijadiliwe na Bunge kama suala la dharula kwani ndani yake kulikuwa na udhalilishaji, unyanyasaji wa hali ya juu na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mwongozo waSpika alioutoa :- Alisema kuwa Kutokana na unyeti na udharula wa suala hilo, basi Serikali ilete majibu kesho bungeni na taarifa ya kilichojiri jana ili bunge lipate fursa ya kujadili.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo ya Spika ilionekana dhahiri wabunge wa upinzani kupitia umoja wao wa UKAWA hawakuridhishwa na hayo maelezo, ndipo walipoamua kusimama na kwa kauli moja wakipaza sauti zao wakisema shughuli za bunge haziwezi kuendelea mpaka hoja yao ya msingi ipate majibu. 

Hali haikuwa shwari ndipo Spika wa bunge Mhe. Makinda akafanya maamuzi. 
ZAIDI SIKILIZA TAARIFA YA RAHEL CHIZOZA KUTOKA DOM.

Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akiwa chini ya ulinzi, eneo la Mtoni Mtongani jijini Dar jana, baada ya  Polisi kusitisha maandamano ya chama chake.
Kabla ya tukio la jana, siku kadhaa nyuma polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.