ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 29, 2014

HII HAPA NGOMA MPYA YA LADY JAYDEE FT DABO - FOREVER


ULIKUWA ukiisubiri kwa hamu ngoma mpya ya Lady Jaydee, au pengine ukijumuika na wengi waliokuwa na maswali kuhusu maisha yake ambapo kwa kinywa chake hivi majuzi alipohojiwa na chombo kimoja wapo cha habari Bongo Tz alinukuliwa akisema kuwa majibu ya baadhi ya maswali ya wengi yatapatikana ndani ya ngoma yake mpya.

Sasa mwanamama Lady Jaydee kaachia kichupa cha wimbo Forever akimshirikisha mshindi wa tuzo za Kilimanjaro katika muziki wa Reggae na Ragga namzungumzia Dabo. Chekshia video hapo juu.

RAIS KIKWETE ASEMA AMEPONA SARATANI

Rais Kikwete akizungumzia afya yake.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.
CHANZO: BBC SWAHILI.

Friday, November 28, 2014

LAMUDI TANZANIA KUTANGAZA HUDUMA ZA MADALALI BURE.

Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Lamudi Tanzania, imetambulisha huduma yake ya kuwawezesha madalali mbalimbali wanaofanya kazi ya kuwatafutia nyumba, viwanja na magari wateja wao ili kuweza kutangaza huduma wanazotoa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma amesema kwa sasa madalali wanaweza kutangaza nyumba, viwanja na magari yaliyoko sokoni kupitia mtandao wa kampuni hiyo bila malipo yoyote.

Akifafanua zaidi Lemma alisema dalali anayependa kupata huduma hiyo anatakiwa kufika katika ofisi za Lamudi Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam (Garden Road) na kujaza fomu ambayo itaelezea huduma yake na kuanza kuitangaza kwenye tovuti www.lamudi.co.tz bila malipo yoyote. “…Kimsingi huduma hii inawasaidia sana madalali kutangaza kazi walizonazo, bei zao na hata eneo ilipo. Mfano kama ni nyumba au kiwanja baada ya dalali kutoa taarifa za kutosha sisi tunamtangazia bure kazi hiyo kupitia tovuti yetu (www.lamudi.co.tz),” alisema Lemma.

Alisema mbali ya kuwasaidia madalali kutangaza bidhaa zao wameanza kutoa pia mafunzo ya kuwajengea uwezo madalali kuweza kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi ili kujenga heshima ya kazi zao. “Wakati mwingine tumekuwa tukifanya kazi ya kuchukua baadhi ya madalali na kuwajengea uwezo, kuwapa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi na masuala mengine ya msingi katika shughuli zao,” alifafanua Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.

Pamoja na hao alisema kwa sasa kampuni ya Lamudi Tanzania imezinduwa huduma mpya ya kumwezesha mteja kupata taarifa za uuzaji au ukodishaji nyumba ama viwanja kupitia simu za mkononi hivyo kumrahisishia kupata taarifa kwa wakati. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

NJOO TUAGE MWEZI NOVEMBA KWA STAILI YA AINA YAKE NA SKYLIGHT BAND IKIWEMO RED CAPET TREATMENT, LEO THAI VILLAGE

DSC_0016
Kutoka kushoto ni Dinga Mbepera, Aneth Kushaba AK47, Sam Mapenzi na Bella Kombo wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki ambapo ratiba ya Skylight Band wiki hii tukifunga mwezi Novemba kwa mwaka 2014 ni kama ifutavyo.

IJUMAA 28.11.14: Kama kawaida tunaaga mwezi aina yake, skylight friday ndani ya Thai village masaki,special show ya mwisho wa mwezi kuwashukuru wadau wetu, Kutakua na Red carpet treatment, kutakua free shots of tequilla mlangoni, zawadi kwa dancers na shabiki wetu wa mwezi atapatikana#si ya kukosa ijumaa hii
JUMAMOSI 29.11.14:Hii ni siku ya bata na bata litaendelea, ni Pale Azura Beach Club Kawe Darajani kwenye siku kuu ya bata#Bata day# muziki na bata, usikosee hii
JUMAPILI 30.11.14: Ni bonanza letu la kistaarabu la kumalizia weekend, Skylight Sunday bonanza#Escape1 beach club# tutamaliza weekend yetu na mziki wa nguvu hii itakua ki africa zaidi#miziki mbalimbali toka barani africa#piga ki africa upate zawadi
DSC_0093
Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower akiwachezesha gwaride wasanii wenzake Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Sony Masamba na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0025
Meneja wa bendi Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0136
Mashabiki wa Skylight Band nao wajisakata sebene la vijana wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0037
Rappa Sony Masamba wa Skylight Band akishusha mistari Ijumaa zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar huku akipewa sapoti na Joniko Flower pamoja na Sam Mapenzi.
DSC_0071
Kipaji kipya ndani ya Skylight Band anafahamika kwa jina la Alice.
DSC_0048
Kijana machachari mwenye sauti ya kipekee Hashim Donode akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akipewa sapoti na Sony Masamba pamoja na Bella Kombo.
DSC_0077
Comme si je n'existais pas..Elle est passé à coté de moi,..Sans un regard, reine de Saba…J'ai dit, Aicha, prends, tout est pour toi... pale shabiki alipokunwa na uimbaji wa Hashim Donode na kuamua kumshusha jukwaani wacheze pamoja.
DSC_0111
Diva Digna Mbepera akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akipewa back up na Sony Masamba pamoja na Hashim Donode.
DSC_0129
Mashabiki wa Skylight Band wakipata burudani kutoka kwa Digna Mbepera (hayupo pichani).
DSC_0145
Twende kazi hakuna kulala hapa.!
DSC_0148
Mashabiki nao walijibu mashambulizi hawajakubali kushindwa.
DSC_0171
Mashabiki wa Skylight Band wakijibu mashambulizi kwa kusebeneka.
DSC_0177
Ehn dorobucci..Don dorobucci…Doro jazzy…Ehn doro boss..Doro big…You know say doro heavy…Doro skillful…You know say doro bloody…Doro get the biggest label wey you..Know of course…Doro tush pass anybody wey doro meet…Doro gather pass anybody for..The gathering…Doro get money pass everybody there.......Unapofika ule muda wa Naija Flava hivi ndivyo Sam Mapenzi anavyowadatisha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0175
Doro na diva....doro…Doro na tiwa..Doro na leader....doro..Follow the leader...doro…Doro doro do do doro....doro…Doro is bigger...doro…Doro is higher…Follow the ladder...doro…So follow the ladder......Na watuache kwa raha zetu.
DSC_0160
Joniko Flower akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0128
Mashabiki wa Skylight Band wakipata ukodak Ijumaa iliyopita.
DSC_0190
Mashabiki wa Skylight Band wakifurahia ukodak.
DSC_0200
Bella Kombo na Emma Beyz wakishow love back stage.
DSC_0153
Mratibu wa Skylight Band, Dean Nyalusi wa ZIFF pamoja na Blogger wa Vijimambo...
DSC_0205
Mashabiki na wadau wa ukweli wa Skylight Band.

Thursday, November 27, 2014

BONUS TRACK- MTOTO WA FISADI BY KINGKAPITA

YULE KIJANA HATARI WA MISEMO ANAETESA NA TRACK YAKE YA 'KUNA TATIZO KWANI' ALIYOMSHIRIKISHA GODZILA, BAADA YA MAMBO YANAYOIENDELEA NCHINI KINGKAPITA AINGIA STUDIO NAKUANDIKA WIMBO HUU NA KUAMUA KUIACHIA KAMA BONUS KUFUNGIA MWAKA - MAALUM KAMA SALAMU KUTOKA GHETO - KITAANI KWA WALE WOTE WANAOKULA HELA ZA JASHO LA WANANCHI - WIMBO UNAITWA MTOTO WA FISADI VS MTOTO WA MTANII.

AKIONGELEA MAISHA YA WATOTO WA MAFISADI NA MAISHA YA MTOTO WA MTAA ALIO RECORD MIAKA MITATU ILIOPITA.

HII NI BONUS TRACK MUDA WOWOTE MTASIKIA NGOMA MPYAAA NA PROJECT KIBAO BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE NJE YA NCHI. BOFYA PLAY KUUSIKILIZA HAPO JUU.

WAFANYAKAZI WA AIRTEL KUWAUNGANISHA WADAU KATIKA KUSAIDIA SHULE YA MSINGI KUMBUKUMBU-Dar

Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi
Wafanyakazi wa Airtel kuwaunganisha wadau katika kusaidia shule ya msingi Kumbukumbu-Dar

·         Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10
·         Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali”imeandaa matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.

Matembezi hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.

Akiongea kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema “wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari ameshachangia.

Na sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri

“Lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”

Tutafanya Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.

Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora ,katika mazingira mazuri  na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa


Airtel chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA KUWA MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU ‘USILIE’ DESEMBA 7/2014

 Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu.
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.

Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
 Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.

Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini.
“Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.

Wednesday, November 26, 2014

KIMENUKA BUNGENI.

PAMOJA na maneno mengi yaliyosemwa, shutuma lukuki zilizotolewa na mbinu za kila aina kutaka kuzuia mjadala wa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL, hatimaye hii leo kila kitu toka kwenye uchunguzi wa kamati kimewekwa wazi jioni hii.


Taarifa ya kamati imeainisha nani mkweli na nani mwongo wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), lilipowasilisha bungeni maoni yake kuhusu ripoti ya kuchotwa kwa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Uchunguzi huo ulifanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa maelekezo ya Serikali baada ya kuombwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alipolalamikia ufisadi huo bungeni.
Pamoja na juhudi za kampuni ya IPTL na PAP kufungua kesi kuzua mjadala huo bungeni, hukumu iliyotolewa jana na majaji watatu ilisema kila kitu kiendelee kama kilivyo na kitakachoendelea kisiathiri kesi iliyopo mahakamani ambapo sasa mambo hadharani.
Moja kati ya MAPENDEKEZO MAKUU yaliyotolewa mara baada ya Taarifa hiyo kusomwa ni:- 
- Kufilisi mali zote za waliohusika ikiwa ni pamoja na hata wale waliohusishwa kwa nia njema.
-Baadhi ya walionufaika na fedha hizo ni viongozi wa Umma ambao wanapaswa kuzingatia sheria ya maadili ya viongozi wa Umma ikiwemo sheria namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka kutoa taarifa ya Zawadi wanazopata au Malipo wanayolipwa. Vyombo vya uchunguzi vitafanya kazi yake kuona kama Matakwa ya Sheria yalifuatwa....
 BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA YA KAMATI 

HUYU NDIYE MSHINDI WA NDOVU GOLDEN EXPERIENCE.

Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya pili ya kampeni ya “Ndovu Golden Experience” yakusaka washindi wa kutembelea hifadhi ya Selous. Amandi Kimario mkazi wa Mbezi alishinda katika droo hiyo. Kushoto ni mwakilishi kutoka bodi ya kubahatisha nchini, Humudi Semvua.
NA MWANDISHI WETU
MSHINDI wa pili ya shindano la Ndovu Golden Experience Amand Kimario amewapiga kumbo washiriki wenzake katika shindano hilo na kujinyakulia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Selous mwakani.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt ambao ndio waratibu wa shindano hilo Pamela Kikuli alisema, lengo la kuandaa shindano hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa Watanzania kutembelea hifadhi na kujivunia utalii wao wandani.

Pamela alisema, mshindi huyo amepatikana baada ya kuchezeshwa droo ambapo yeye aliwabwaga wenzake waliojitosa katika shindano hilo, ambapo atatarajiwa kuwana mwenzake ambaye wataongozana katika hifadhi hiyo.

Alisema, kwa kutambua bia yao ya Ndovu inabebwa na nembo ya mnyama Tembo, wanatumia nafasi hiyo kumlinda mnyama huyo kama kampeini yao inavyosema 'Ndovu Defance', ilikunusuru mauaji yake.

"Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania, ila utalii mkubwa unaofanyika hapa Tanzania niwa wageni wa nje, hivyo basi tunaamini kwa kuendeleza kampeini yetu hii ya Ndovu Golden Experience, inayoendeshwa kwa kutumia namba za chini ya kizibo, itawapa fursa muhimu watanzania kujivunia utalii wao,"alisema Pamela.

Aidha Pamela alisema, baada ya kumalizika kwa droo ya shindano hilo Disemba 18, washindi wataenda kutembelea hifadhi hiyo Januari mwakani huku wao Ndovu wakigharimia malazi, chakula pamoja na usafiri na kuwataka watanzania kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo kwa kuandika namba chini ya kizibo kwenda namba 15499 au katika mtandao wa www.ndovuspecialmalt.com.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa la kuchochea mwamko wa nafasi ya mabingwa wa uchunguzi tiba katika kuboresha huduma za tiba. Kongamano hilo linalofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, limewakutanisha mabingwa wa tiba za afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika. Picha na OMR
baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano hilo leo Novemba 26, 2014. Picha na OMR
baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano hilo leo Novemba 26, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi waratibu wa Kongamano hilo wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach leo Novemba 26, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano hilo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi waratibu wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR

KAMPUNI YA KONYAGI YANYAKUWA TUZO MBILI ZA ULIPAJI KODI BORA NCHINI

Mkurugenzi wa Fedha wa TDL, Bwana Michael Brown (KUSHOTO) akipokea Ngao ya ushindi kwa TDL baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kama Mlipa Kodi Bora katika kundi la Viwanda, na Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Bw Kigoma malima ndie anaemkabidhi tuzo hiyo.  KONYAGI ilinyakuwa tuzo mbili za ulipaji kodi bora.
Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Mlipa Kodi Bora katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention centre Wengine katika Picha ni Joseph Chibehe meneja mauzo na Edward Mashingia meneja wa Fedha.
 Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown akiwa na tuzo aliyoipokea. 

Maofisa mbalimbali wa makampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za ulipaji kodi bora nchini.
 Joseph Chibehe meneja mauzo wa kampuni ya KONYAGI kushoto akibadilishana mawazo na Ofisa wa TBL ambao nao walinyakuwa tuzo.
Baadhi ya washiliki walionyakua tuzo za ulipaji kodo bora wakitoka ukumbini na tuzo zao.

Tuesday, November 25, 2014