ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 8, 2014

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AZUNGUMZA NA WANAHABARI MJINI IRINGA LEO KUHUSU

 Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga, ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka huu.
Pichani wa tatu kulia ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga, ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka huu.Shoto ni Bwa.Mihayo Kadete,Erald Martin na kulia ni Isaya Makoko ambao wote ni Maofisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano uliondaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga mapema leo asubuhi,na pia Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa kujtambulisha uwepo wake katika zoezi zima la uchaguzi wa Kalenga sambamba na kuwafahamisha Wananchi zinazofanywa na Ofisi za Msajili wa vyama vya siasa tangu Maafisa wa Ofisi hiyo wafike mjini Iringa.
Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akifafanua jambo kwa Wanahabari mapema leo asubuhi,mkoani Iringa.MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-IRINGA

KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LTD. KONYAGI WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.


Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd. | Konyagi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa march 8 kila mwaka


Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd.  Konyagi wakiwa katika maandamano yaliyoanzia ofisini kwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyoadhimishwa march 8 kila mwaka


Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd. |Konyagi wakiwa katika maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyoadhimishwa march 8 kila mwaka na kuishia katika viwanja vya mwembeyanga Dar es salaam

Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd.  Konyagi wakiungana na wanawake wenzao kutokasehemu mbalimbali kuadhimisha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika viwanja vya mwembeyanga Dar es salaam

Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd. | Konyagi wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanawake wenzao katika viwanja vya mwembe yanga Dar es salaam  wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa March 8 kila mwaka

Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd.  Konyagi wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanawake wenzao katika viwanja vya mwembe yanga Dar es salaam  wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa March 8 kila mwaka

Friday, March 7, 2014

VITU VYA HUMU HUMU MAZEE!!!

Matayarisho ya Migebuka, katika soko la Msufini mkini Kigoma.
Juu kwa juu Kigoma.
Engo nyingine mji wa Kigoma.
Sasa safiri kuelekea kisiwa cha Saa Nane ndani ya ziwa Victoria jijini Mwanza njiani utakutana na maadhari haya.
Eneo jingine nchi kavu Mwanza Tanzania. 

NMB WAJA NA LIPIA 30% PATA KITU KIPYAaaa!!

Yawezekana hujapata nafasi ya kusoma mabango yanayopatikana kandokando mwa barabara, lakini kwa ufupi ni kuwa Benki ya NMB hivi sasa inaendesha zoezi la kutoa mkopo kwa wateja wake walio au wanaohitaji kuwa wajasiliamali wa vyombo viwili vya usafiri, nazungumzia Bajaji (pikipiki za miguu mitatu) na Bodaboda (pikipiki) , ambapo unapewa mkopo na kukimiliki chombo chako cha usafiri ukilipia asilimia 30 ya gharama za manunuzi ya chombo kimoja wapo. 
Ni nafasi sasa kuchangamkia fursa hiyo ili kujiongezea mtaji.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0714150660 au 0765700500.

WAKUU WA MAMLAKA ZA BIMA AFRIKA MASHARIKI WAKUBALIANA KUWA NA BIMA MOJA.

Mwenyekiti wa EAST ARFICA INSUARANCE SUPERVISORS ASSOCCIATION (EAISA) na Kamishina wa Bima wa Uganda, Alhaj Ibrahim Lubega Kaddunabbi akiongoza kikao cha wakuu wa Mamlaka za Bima kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kilichoketi katika ukumbi wa Ray's Bay jijini Mwanza, kujadili na kupitisha uamuzi wa kuanzishwa utolewaji wa pamoja wa Huduma za Bima kupitia Makampuni ya Bima kutoka nchi tano wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kamishina wa mamlaka ya Bima nchini Tanzania Israel Kamuzora akishiriki kutoa mchango wake kwenye kikao cha wakuu wa Mamlaka za Bima kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kilichoketi katika ukumbi wa Ray's Bay jijini Mwanza, kujadili na kupitisha uamuzi wa kuanzishwa utolewaji wa pamoja wa Huduma za Bima kupitia Makampuni ya Bima kutoka nchi tano wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mr. Jonathan Gatera ambaye ni mwakilishi wa Gavana wa Benki ya Rwanda, Mrs. Agnes Ndirangu ambaye ni mwakilishi wa kamishina wa Bima wa Kenya, Mwenyekiti wa EAISA na Kamishina wa Bima wa Uganda, Alhaj Ibrahim Lubega Kaddunabbi na kulia ni mwakilishi kutoka Burundi Mr. Venant Kamana.
Mwenyekiti wa EAISA na Kamishina wa Bima wa Uganda, Alhaj Ibrahim Lubega Kaddunabbi akifafanua jambo mbele ya waancdishi wa habari (hawapo pichani).


Mwenyekiti wa EAISA na Kamishina wa Bima wa Uganda, Alhaj Ibrahim Lubega Kaddunabbi akifafanua jambo mbele ya waancdishi wa habari (hawapo pichani). Wengine pichani ni Mrs. Agnes Ndirangu ambaye ni mwakilishi wa kamishina wa Bima wa Kenya (kushoto) na Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini Tanzania Israel Kamuzora.
Akishiriki kuelezea uzoefu wa nchi yake katika utoaji wa Bima Mrs. Agnes Ndirangu ambaye ni mwakilishi wa kamishina wa Bima wa Kenya alisema taifa hilo lina kitengo maalum cha kukusanya na kusikiliza malalamiko na changamoto mbalimbali za Bima kutoka kwa wananchi ikiwemo Bima ya Afya ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora. 
Waratibu wa kikao hicho kikazi zaidi.

WAKATI upatikanaji wa huduma ya Afya kupitia Mfuko wa Bima unaonekana kusuasua hapa nchini na wananchi wengi kusita kujiunga na mfuko huo kutokana na adha na usumbufu wanaoupata kwenye Idara a Afya pindi wanapohitaji kupatiwa matibabu wakiwa na Kadi za Bima ya Afya, hali ni tofauti kwa nchi za zingine zilizopo Jumuia ya Afrika Mashariki.

Hilo limebainika jana Jijini Mwanza katika Kikao cha Wakuu wa Mamlaka za Bima kutoka nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichoketi kujadili na kupitisha uamuzi wa kuanzishwa utolewaji wa pamoja wa Huduma za Bima kupitia Makampuni ya Bima  kutoka nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa kupitisha uamuzi huo Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini Tanzania Israel Kamuzora alisema kuwa bado zipo kasoro katika huduma inayotolewa kupitia Mfuko wa Bima ya Afya nchini kuonekana kusuasua kutokana na wataalamu wa Idara za Afya za serikali na binafsi kushindwa kutoa kipaumbele kwa wananchi walio na Kadi kupatiwa matibabu sawa na watu wengine wanaolipia gharama.

“Mfuko huu hapa nchini umeonekana kama vile watu waliojiunga kama vile ni msaada wakati katika mataifa mengine ya Ulaya, Amerika na Asia na baadhi Barani Afrika bila kuwa na Kadi ya Bima hupatiwi matibabu na Daktari au Mtaalamu lakini hapa kwetu wataalamu wanauliza kuwa analipia gharama ukijibu ndiyo unaanza kutibiwa na kudai una kadi unaelezwa subiri kwanza hili siyo sawa.”alisema.

Kamishna Kamuzora alisema kwamba bado serikali inatakiwa kutoa elimu kwa wataalamu na viongozi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwamba wananchi wenye Kadi za Mfuko wa Bima ya Afya wapatiwe matibabu bila kujali kuwa na fedha tasilimu  huku pia ikidaiwa kuwa wanachama wengi wa mfuko huo hulalamikia usumbufu kwa kuelezwa na wataalamu wa Idara ya Afya baadhi ya vipimo havilipiwi na mfuko huo.

“Nchi zilizoendelea ukienda kwa Daktari na pesa anaweza kukukataa kukupatia matibabu kwa kuwa anatambua kuwa hutoweza kumlipa lakini ukiwa na Kadi atachangamka kukupatia huduma ya matibabu mara moja (First Class) kwa kutambua kuwa Kampuni ya Bima wanao uwezo wa kumlipa gharama za kutibu kutokujua kwetu isiwe ndiyo utaratibu, hivyo elimu iendelee kutolewa kwani sasa imeanza kueleweka” alisisitiza.

Kamzora aliongeza kuwa kwa sasa hapa nchini wananchi wameanza kuchangamkia zaidi wakiwemo walimu ambao awali waliweka mgomo na kukataa kukatwa mishahara yao ili kuchangia mfuko huo lakini hali ni tofauti kwa sasa wengi wao wanaisifia na kuwahamasisha wengine na wananchi kujiunga na mfuko huo lakini leo ukijaribu kuigusa kuwaondolea Bima ya Afya wengi wao watagoma kutokana na kuelewa faida zake.

“Japo itachukua muda kwani tumeelewa tuliko toka na hata kwenye Hospitali zetu wameanza kulitambua hilo lakini kikubwa zaidi ni kuhakikisha elimu inazidi kutolewa na kuwafikia walengwa ili kusaidia wengi kujiunga na mfuko huo wa Bima ya afya ili kupatiwa matibabu bila kunyanyaswa na itafikia wakati hata hao wa kulipia gharama kwa fedha tasilimu watapata usumbufu kutokana na Teknolojia”alisema Kamishna Kamzora.

Naye Jonathan Gatera ambaye ni Mwakirishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Rwanda alisema kwamba kwa serikali ya  nchi ya Rwanda katika utoaji wa huduma ya Afya kwa wananchi wake inazingatia wale walio na Kadi za Bima ya Afya na serikali imekuwa ikihamasisha kwa kutoa elimu na asilimia kubwa wamejiunga na hutumia kupatiwa matibabu mpango ambao umekuwa na mafanikio makubwa.

Mjumbe kutoa Kenya, Agnes Ndirangu ambaye alimwakirisha Kamishna wa Bima wa nchini hiyo alisema kwamba Taifa hilo lina kitengo maalumu cha kukusanya na kusikiliza malalamiko na changamoto mbalimbali za Bima kutoka kwa wananchi ikiwemo Bima ya Afya ili kuboresha meanzisha upatikanaji wa huduma bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Mamlaka za Bima kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Alhaj Ibrahim Lubega Kaddunabbi alisema kuwa kikao hicho kilichoketi kwa siku mbili kilikuwa kujadili na kupitisha maamuzi ya kuifanya Bima itumike kwa nchi zote wanachama wa Jumuiya hiyo badala ya kila nchi kuwa na utaratibu wake wa utohaji huduma za Bima na Viwango tofauti.

Alhaji Kaddunabbi ambaye ni Kamishna wa Bima wa nchini Uganda alisema kwamba lengo la kikao hicho ni kuhakikisha Makampuni ya Bima kushirikiana kwa pamoja kutoa huduma za Bima kwa pamoja badala ya kuwa na Bima ya kila nchi jambo ambalo limekuwa kero na adha kubwa kwa wananchi wanapoamua kutembelea nchi nyingine na kupata usumbufu wa kukata Bima upya ili kuruhusiwa kuingia nchi nyingine.

“Kwa sasa ukiwa na gari lako na BIMA ulilokata nchini Uganda ukienda nchini za Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi haitambuliki, tunalazimika kukata Bima tofauti, huu ni usumbufu ni vyema tukawa na utaratibu wa Makampuni na Mashirika ya Bima kutoa huduma hiyo na kukubalika na nchi zote wanachama, hata ukitokea umepata ajali basi upatiwe matibabu ukiwa nchi nyingine kwa Bima uliyokata nchi nyingine” alisema.

Katibu wa Wakuu wa Mamlaka za Bima (East Afrika Insurance Superviors Assocciation) kwa kifupi inafahamika EAISA, Venant Kamana kutoka nchini Burundi alisema kwamba Makampuni hayo ya utoaji wa Bima endapo yatafikia uamuzi wa kutoa huduma za pamoja kwa kushirikiana haitoathiriwa na uthamani wa fedha kwani Mabenki yaliyopo kila nchi yatatumika viwango vinavyojulikana kimataifa katika ubadilishaji wa fedha toka nchi moja hadi nchi nyingine za Jumuiya.

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUMWAGA RAHA KWA MASHABIKI WAKE, NI IJUMAA HII TENA @ Thai Village

DSC_0031
Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani Ijumaa iliyopita kwa mashabiki wao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar... Burudani inaendelea kama kawaida tukutane tena leo jioni......ni balaaaaa..!
DSC_0019
Divas wa Skylight Band... Kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47 wakikonga nyoyo za mashabiki wao ndani ya kiwanja chao cha nyumbani Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0037
Rapa Joniko Flower akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani ya aina yake Ijumaa iliyopita.
DSC_0062
Mpiga Tumba wa Skylight Band Daudi akifanya yake jukwaani...!
DSC_0071
Hela yako haipotei bure kwa burudani kama hii... ni balaaa...!
DSC_0098
Sam Mapenzi akipagawisha mashabiki wa Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita...Pichani ni mdau Alois Ngonyani akionekana kukunwa na uimbaji wa kijana Sam Mapenzi.
DSC_0093
Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo akiburudika na mmoja wa mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0083
DSC_0113
Muziki wa pwani a.k.a mduara ulihusika pale kati.
DSC_0121
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga na mduara.
DSC_0125
Palikuwa hapatoshi hapo kati.
DSC_0072
Wadau wa Skylight Band wakishow love na Ukodak.
DSC_0126
Mwanafamilia wa Skylight Band Victor Maginga (kulia) akiwa na DJ Peter Moe pamoja na mdau wakipata Ukodak.
DSC_0094
Aneth Kushaba AK47 akishow love na washirika wakubwa wa Skylight Band Alois Ngonyani (katikati) pamoja na Emmanuel Francis.