ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 25, 2014

TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8JANUARY) LAFANA MJINI MOROGORO

 Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

Tuo8January ni kampeni maalum iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

Kama vile haitoshi kampeni hiyo inatumika kuwahamasisha vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi kuchukua hatua sasa za kufanya hivyo,pia kupata vijana wen,vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu na kuwa vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha mambo ya msingi yanajadiliwa na wagombea na yanapewa kipaumbele. 

Katika tamasha hilo Fid Q aliwahamasisha vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye tamasha hilo,kuwa imefika wakati wa vijana kujitokeza kushiriki mambo mbalimbali ya kimsingi kwa manufaa ya nchi yao na si kukaa chini na kuanza kulalama,wakati kwenye mambo ya maamuzi wakishirikishwa hawataki kujitokeza,hivyo ni wakati wao wa kuamka na kuchagua kiongozi kijana wa kisasa na si kiongozi wa kisiasa.
 Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
 Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini Dar hivi karibuni na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo,akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto,G-nako,Fid Q,Shilole,Yamoto Band,Stamina na wengineo.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Tuon8January katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro.
 Ilikuwa ni shangwe tu kutoka kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kupitia tamasha la Tuo8January
 Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya,aitwaye Stamina akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro katika tamasha la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
 Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
 Baadhi ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.

 Pichani kulia ni Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka akiungwa mkono na shabiki wake kwa kunogesha zaidi jukwaa,huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki waliofika katika tamasha la Tuo8January hapo jana.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
 watazajamaji wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la Tuo8January hapo jana katika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.
 Mkali mwingine wa kufloo freestyle,Godzilla akipanda katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,tayari kwa kuwaburudisha wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.