ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 17, 2014

KUMBUKUMBU

MAREHEMU  NDUGU  CLEMENT  MABINA
Mwanaume, baba, babu, mjomba, kaka, mwana, ndugu na rafiki wa wengi
Ulikuwa mtu mwema, mkarimu, mwenye upendo na mcheshi sana!

Rafiki uliyeaminika, uliyetegemewa, muungwana na ulikuwa mkweli sana!
Mtu wa watu, jasiri uliyejitolea kwa bidii bila kuchoka-  uliwasaidia wengine, hasa waliohitaji msaada zaidi. Hukubagua itikadi, kabila, chama, dini, rangi, elimu, wala uwezo

Ulikuwa kiongozi muelewa, mchapakazi na mwenye hekima,
Yaani kwa kweli maneno pekee hayatoshi kukuelezea ulivyotugusa wengi

Binadamu sote hatuja kamilika
Ulikuwa binadamu wa kawaida tu ila pia wakipekee
Mwenye maono, upeo wa mbali na matumaini ya maendeleo kwa wote
Uliamini kwa moyo wako wote kabisa katika uhamasishaji wa uhifadhi na udumishaji wa utamaduni wa kiafrika
Picha: Wakati bado yu hai, Clement Mabina Akishirikiana na kuhamasisha
sherehe zaUtamaduni za ‘Bulabo’ ndani yaBujora , Kisesa. 
" Shilikare omukaya atena Magaka " 
" Polisi wa Nyumbani aheshimiki "
  
Clement ,ki-binadamu maisha yako kwa sasa yamemalizika, lakini mwanga wako, nafsi yako na upendo wa kudumu utaangaza duniani hapa milele, katika mioyo ya wote ambao wewe uliwagusa kimaisha
Umetoweka, lakini kamwe hutasahaulika
Maana pia maandiko matakatifu yanatufariji kwa njia gani na kwa njia gani Kristo alikufa

MWAKA  MMOJA  ULIOPITA,  ASUBUHI   KWENYE  MAZISHI  YA
MAREHEMU  NELSON  MANDELA
MAISHA  YAKO  YALIKATWA  KIKATILI NA  KIAJABU  SANA
MUNGU  ANAJUA  HAUKUSTAHILI  KUFA  KIFO CHA  AJABU  HIVYO
WALE WALIOHUSIKA,  MPAKA LEO, BADO  HAWAJAKABILIWA
KISHERIA
HAKI  BADO  HAIJATENDEKA

Tuna mlilia na kumuomba Mungu; muona vyote na mfahamu vyote
Kila haki na ukweli kutoka kwa Mungu ujidhihirishe kwa wote
Eh Mola, wewe ni nanga, nguvu na kimbilio letu

Clement, tunakukumbuka sana!
Kwaheri mpendwa wetu
Mpaka tutakapo kutana tena


PUMZIKA  KWA  AMANI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.