ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 23, 2014

KENYA YAUWA AL-SHAHBAAB 100.

Mashuhuda nchini Kenya wakiranda karibu na basi ambalo abiria wake walikumbwa na uvamizi na kuuawa na kundi la Al-Shabaab jana Nov. 22, 2014. PICHA NA 
CHANZO/BBC.
Makamo wa rais wa Kenya, William Ruto, anasema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi kaskazini-mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 waliuliwa.
Bwana Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni mbili tofauti.
Alisema kambi ya al-Shabaab iliangamizwa.
Habari hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Miili ya abiria waliouawa mara baada ya uvamizi huo kutokea jana Nov 22, 2014 nchini Kenya. PICHA NA 
Gavana wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuwalinda raia.
Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.