ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 30, 2014

SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI PROGAMU YAKE YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” KWA MSIMU IV, 2014.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akiwaonyesha kipeperushi cha shilingi 2200,000 000/= zitakazogawiwa kwa wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa prpgramu ya Safari Wezeshwa msimu wan ne uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji wa programu hiyo, Joseph Mmigunda.
Jaji wa programu Safari Wezeshwa kutoka Kampuni ya TABDS, Joseph Mmigunda(kulia)  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa program hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo

SAFARI LAGER YAZINDUA  RASMI  PROGAMU YAKE  YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” KWA MSIMU IV, 2014.
Dar es Salaam, Alhamisi  Oktoba 30 2014: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imeziduwa rasmi programu yake ya Safari  Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo Nchini.  

Akizungumza  na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo  alifafanuwa ya kwamba “ programu hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi  kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.

Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na  imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.

Bw. Oscar alifafanuwa kuwa, Programu hii itafanyika takribani mikoa yote Nchini ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo kupitia mtandao wa www.wezeshwa.co.tz na baadae kusambazwa katika mabohari na viwanda vya TBL nchi nzima.Hii itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi  pamoja na kukabidhiwa ruzuku  zao.

Nae Jaji kutoka TABDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa  “Zoezi hili linahusisha majaji wenye utaalamu na  wenye umakini  kwa namna moja au nyingine.Hivyo aliomba wajasiriamali wote wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye  malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.