ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 23, 2014

MWANZA COMMERCIAL COMPLEX KIVUTIO KINGINE CHA AINA YAKE.

Mtangazaji wa Aplifaya toka radio Clouds Fm Millard Ayo akiripoti toka eneo la tukio, katika safari yake aliyoifanya miezi miwili iliyopita akijumuika na G. Sengo Blog kutembelea eneo la uwekezaji Mwanza Commercial Complex.
HUU ni ujenzi wa mradi wa ujenzi Soko la Kisasa la Mwanza (Mwanza Commercial Complex), ambao tayari umekwishaanza takribani miaka miwili sasa na umefikia katika hatua hii nzuri.

Mradi huu wa ujenzi wa kitenga uchumi hiki, unaendeshwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakati Jiji hilo halijagawanywa kuwa pande mbili, na Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF). Mradi huo unajengwa eneo la Ghana, katika Kata ya Nyamanoro iliyoko ndani ya mipaka ya Manispaa ya Ilemela.

Watanzania wazalendo wa nchi hii ndiyo watakao pewa kipaumbele kuwekeza biashara katika mradi huu wa mwanza Commercial Complex.

Na mradi huu, hadi utakapokamilika, unakadiriwa kugaharimu Sh bilioni 60.45.
Milango ya jengo hili iki katika mwonekano wa mdomo wa samaki.
Kwandani eneo la katikati.
Juu kabisa eneo la katikati
Lifti.
Ngazi za umeme.
Ngazi za umeme kutoka eneo moja hadi jingine.
Mwonekano wa moja kati ya flow.
Eneo maalum kwaajili ya parking.
G
Sakafu ya parking.
Kutoka sakafu ya eneo la kuegesha magari (parking) hadi mjengo wenyewe wa Mwanza Commercial Complex  
Ramani ya mjengo utakapo kamilika miezi kadhaa ijayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.