ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 29, 2014

DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA 5 LA KIMATAIFA KUJADILI MATUMIZI YA NISHATI ITOKANAYO NA JOTO ARDHI KATIKA NCHI ZA AFRIKA ZINAZOPITIWA NA BONDE LA UFA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. Picha na OMR
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili ya kabila la wamasai wakati akiondoka katika Ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo. Picha na OMR

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.