ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 22, 2014

KEKUNDU WAPATA SHAVU KUTUMBUIZA SHEREHE ZA UHURU DEC 9.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kwaya ya AICT Vijana Makongoro .
Kwaya ya AICT Vijana Makongoro  wakiimba wimbo wa 'Usiichezee amani'

NA PETER FABIAN, MWANZA.
AIC MAKONGORO VIJANA KWAYA 'Wana Kekundu' wanaotamba hivi sasa na album yao mpya ya  “KEUSI” toka Kanisa la African Inland Charch (AIC) ya Makongoro yamkosha Rais Dkt. Jakaya Kikwete, kwa nyimbo za Amani na Tukae mezani na kuialika kutumbuiza kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru, Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo ya Rais Dkt. Kikwete kuialika kwaya hiyo inafuatia hivi karibuni akiwa jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ya kuzindua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Usagara–Kisesa yenye urefu wa km 16, ilipotoa ujumbe huo wa nyimbo za Amani na Tukae mezani kumaliza tofauti zetu.

KEKUNDU AIC Vijana Kwaya ilitoa ujumbe huo kwa nyimbo mbili katika viwanja vya Mabatini Polisi baada ya Rais Dkt Kikwete na ujumbe wake kuzindua daraja la Mabatini na kisha kwenda kuhutubia wananchi kwenye viwanja vya Polisi Mabatini na kabla ya viongozi kuanza kuhutubia ilipopata nafasi ya kutoa ujumbe huo.

Mamia ya wananchi waliofurika wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi, vyama vya siasa na wadau wa maendeleo, kuwa katika hali ya utulivu kusikiliza ujumbe huo hali iliyoonekana kumgusa kila mmoja kwa jinsi kwaya hiyo ilivyowasilisha kwa hisia na hata kumkosha Rais Dk Kikwete na ujumbe wake huku wananchi wakishangilia kwa kupiga makofi.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Rais Dkt. Kikwete, alisema nawapongezeni Vijana  Kwaya kwa njisi mlivyo tukumbusha watanzania wote juu ya kuendelea kulinda amani ya taifa hili na kamwe tusiichezee kwani ikitoweka hatuta ipata tena na wimbo wa tukae mezani kuzungumza na kujadiliana tofauti zetu na si vinginevyo.

“Asanteni kwa ujumbe wenu mzuri uliojaa maneno ya kuwakumbusha watanzania juu ya amani, hivyo nawaalika mje kutoa ujumbe huu tena kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru Desmba 9 mwaka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salamu, hakika nimefurahi,”alisisitiza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.