ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 17, 2014

TOTO AFRICANS KUKIPUTA NA MABINGWA WA UGANDA VIPERS KESHO ALHAMISI DIMBA LA CCM KIRUMBA

Mabingwa wa Uganda Vipers Sc.
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Katika kujiweka sawa na mikikimikiki ya ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara kupata ushindi na hatimaye kurejea Ligi Kuu ya Premium, timu ya soka ya Toto Africans (Wanakishamapanda) ya jijini Mwanza inajinoa katika hatua za mwisho kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers Football Club utakaochezwa 'KESHO' tarehe alhamisi hii ya tarehe 18 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Kaimu Mwenyekiti wa Toto Africans Dr. Keneth Petro (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia maandalizi ya mchezo wa Toto Africans v/s Vipers Sc ya Uganda utakaochezwa alhamisi ya wiki hii dimba la CCM Kirumba Mwanza. Wengine katika picha ni Katibu wa klabu hiyo Issack Mwanahapa (katikati) na Catherine kahabi ambaye ni maratibu wa Mchezo huo unaoletwa chini ya Uongozi wa Mbeya City. 
Kocha Mkuu wa Toto Africans John Tegete (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia maandalizi ya timu ya Toto Africans itakayoshuka dimbani CCM Kirumba Mwanza, alhamisi hii ya tarehe 18 kucheza na Vipers Sc ya Uganda.
Kaimu Mwenyekiti wa Toto Africans Dr. Keneth Petro anasema mchezo huo ni muhimu kwa klabu yake ambayo licha ya kufanya maandalizi makubwa katika usajili ili irejee ligi kuu, vilevile klabu yake yenye jina kubwa nchini, ina malengo mapya yenye sura mpya ya kurejea ligi kuu na kuutwaa uchampioni wa ligi hiyo hatimaye kuelekea Michuano ya Kimataifa. 

Zaidi huyu hapa  (BOFYA PLAY KUSIKIA MZUNGUMZO)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.