ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 21, 2014

TAMASHA LA COCE STUDIO KUNYWA COCA UJEPATIE MUDA WA MAONGEZI WA DAKIKA 5 PAPO HAPO

Meneja  masoko wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca kanda ya ziwa Marco Masaka akizungumza juu ya uzinduzi wa  promosheni mpya,  ambao umefanyika katika viwanja vya kampuni hiyo jijini Mwanza.
Masaka amesema kama watanzania watakuwa na utamaduni wa kushiriki katika matamasha mbalimbali  kwa namna moja ama nyingine ana amini watapata manufaa zaidi.
Hata hivyo Marco Masaka ametoa mwito kwa wakazi wa kanda ya ziwa na Watanzania kwa ujumla kuona umuhimu wa kushiriki tamasha hilo ambalo nila miezi miwili na nusu kwani ni sawa na matamasha mengine ambayo yanaendeshwa na kampuni hiyo. 
Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili kwa kampuni hiyo kuandaa promosheni  yenye lengo la kuwaweka watu pamoja kwa njia ya kiburudisho na mawasiliano kupitia kinywaji cha coca cola chenye kizibo cha rangi ya njano.
Jinsi ya kushiriki ili upate dakika 5 za bure za kuongea, kuchati na kuperuzi mtandao wa Vodacom.
Mirindimo ya burudani.
Watu na vinywaji vyao.
Kuanzishwa kwa Matamasha mbalimbali nchini ni njia mojawapo ya kuwapa fursa Watanzania kushiriki na hatimaye waweze kujikwamua na umaskini.
Hii inatokana na baadhi ya Makampuni kuanzisha na kuendesha matamasha yenye jumbe tofauti ikiwemo Kampuni ya Coca Cola.
Meneja  masoko wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca kanda ya ziwa Marco Masaka akizungumza na wateja ambapo kulikuwa na fursa pia ya maswali na majibu kwa dakika kadhaa.
Mwezi Juni mwaka huu baadhi ya watanzania walipata fursa ya kushiriki shindano la jionee mwenyewe kombe la FIFA la Dunia na Coca Cola 2014  nchini Brazil ambapo walijinyakulia tiketi ya kwenda kushuhudia fainali za kombe la dunia nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.