ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 1, 2014

MOROGORO, IRINGA NA MBEYA WAPATA MABINGWA WA SAFARI POOL 2014

Mweka hazina wa Chama cha pool taifa (TAPA), Zaholo Ligalu (kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya klabu ya Anatori ya Morogoro pesa taslimu Shilingi 800/000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mchezo wa Pool unajulikana kama “Safari National Pool Competition 2014”  ngazi ya mkoa, mkoa Mkoa wa Morogoro uliomalizika mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wa klabu ya Anatory ya Morogoro wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa, mkoa wa Morogoro uliofanyika DDC mjini Morogoro.
Morogoro, Iringa na Mbeya wapata mabingwa wa Safari Pool.

Na Mwandishi Wetu.
KLABU ya Anatory ya Morogoro, Ngija Masters ya Iringa na Break Point ya Mbeya zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mikoa katika fainali za mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya Mikoa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mikoani humo na kuzawadiwa kila klabu fedha taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Kwa matokeo hayo ya mikoa mitatu ndipo mtanange wa kuwatafuta mabingwa kutoka katika mikoa 17 inayoshiriki fainali za mashindano ya Safari Pool 2014 unafungwa rasmi na tunaelekeza nguvu na masikio kwenye fainali za kitaifa Septemba 14 mwaka huu.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Morogoro, Bingwa mtetezi wa mkoa, Mussa Mkwega alitetea vyema ubingwa wake, Iringa ni Godlove Chalangwe ndiye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa wakati Mbeya ni Majali wa Sipilian alitwaa ubingwa wa mkoa wa huo na kwa ubingwa huo kila mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume.

Mchezaji mmoja mmoja Wanawake waliofanikiwa kutwaa ubingwa ni, Morogoro, Bingwa mtetezi Rosemary Deus alitetea vyema ubingwa wake, Iringani Naomi Ngede alitwaa ubingwa wakati jijini Mbeya ni Happness Robert ndie alitwaa ubingwa wa mkoa na kwa ushindi huo kila mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake.

Fainali  za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora, Shinyanga, Dodoma Mbeya, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha, Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.