ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 23, 2014

FIFA YAANZA KUUKARABATI UWANJA WA NYAMAGANA.

 NA ALBERT G. SENGO, MWANZA:

BAADA ya kipindi kirefu cha wapenzi wa soka wa mkoa wa Mwanza kuwa na kiu ya kutaka kuuona uwanja wao wa Nyamagana ukianza kufanyiwa ukarabati na kuwa na hadhi, hatimaye  Mkandarasi wa ujenzi na kuweka Nyansi ameanza kazi yake rasmi baada ya kukamilisha taratibu zote.

TFF imekamilisha mchakato huo na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) ambapo imemteuwa Mkandarasi Kampuni ya JASSIE Ltd ya Jijiji Mwanza kufanya kazi ya ujenzi wa majukwaa atakaye shirikiana na Mkandarasi aliyeteuliwa na FIFA wa kazi ya uwekaji nyansi kufanya kazi hiyo chini ya wataalamu wa viwanja wa FIFA kwa kushirikiana na wale wa waliteuliwa na TFF toka mkoa husika (Mwanza) BOFYA PLAY KUSIKILIZA MAHOJIANO. 

Wakandarasi wakiendelea na kazi ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Shughuli ikiendelea.
Mafundi waking'oa magoli yaliyokuwepo kwenye uwanja huo kwaajili ya kupisha ukarabati unaofanyika kuweka nyasi za bandia sambamba na kutengeneza majukwaa..
Tabaka la juu la uongo kwa kina fulani linaondolewa.
Shughuli ni kona hadi kona.
Hali halisi kona na kona.
Engo na engo.
Ukarabati huu umekuja mara baada ya Mamlaka za Mkoa wa Mwanza kutimiza ahadi yao ya kuchangia dola 118,000 za Marekani (zaidi ya sh. milioni 190) ili kukamilisha mradi wa kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza zoezi ambali lilifanyika mwezi Oktoba mwaka jana (2013).

Chini ya mwamvuli wa TFF, Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Hassan Hida walisimamia mpango huo mpaka kikaeleweka, ambapo sasa shughuli imeanza rasmi ikitarajiwa kukamilika mapema mwakani.


G. Sengo Blog inakuahidi kuendelea kukupatia taarifa mbalimbali, hatua kwa hatua juu ya yale yanayojiri toka katika eneo hili la uwekezaji, uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.