ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 18, 2014

DC KONISAGA AKABIDHI SARUJI MIFUKO 500 KWA MEYA MABULA KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA.


NA PETER FABIAN, MWANZA.

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, amepokea mifuko 500 ya saruji sawa na tani 25, ambayo ameikabidhi kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa maabara 68 za jiji hilo.

Akizungumza jana katika hafla fupi ya kupokea na kukabidhi msaada huo wa saruji, konisaga alisema msaada huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanza Huduma, Zurry Nanj , ambaye ni Wakala wa kuuza na kusambaza saruji ya Kampuni ya Twiga mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Tangu Rais Jakaya Kikwete atoe agizo kwa sisi wasaidizi wake kusimamia kila sekondari kuwa na maabara tatu , tumekuwa tunahangaika kuhakikisha tunatekeleza agizo hilo kwa ujenzi wa maabara hizo hivyo tumepata msaada huu wakati muafaka ambao utasaidia kukamilisha ujenzi,”alisema.

Konisaga alisema msaada huo wa Nanj ameutoa baada ya kufika ofisini kwake kumweleza harakati za ujenzi wa maabara katika shule za sekondari 30 zilizopo katika Kata 12 za Wilaya ya Nyamagana, alikubali kuchangia saruji na kudai siyo mwisho na amekusudia kuendelea kutusaidia kadri atakavyoweza.
“Hii ni mara ya pili kwa mudau huyu wa maendeleo kuchangia saruji kwani mwezi Mei mwaka huu alichangia mifuko 300 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi za Kata za Igogo, Butimba, Igoma na Buhongwa pamoja na Chuo cha CUHAS cha Bugando hivyo ni mdau wa maendeleo na ameahidi kutusaidia”alisema.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, alisema kwamba Halmashauri hiyo imekwisha jenga maabara 22 za awali na inaendelea na ujenzi wa maabara 68 kukamilisha idadi ya jumla ya maabara 90 zinazohitajika kwenye Kata zote 12 za jiji hilo kama ilivyoelekezwa na Rais Kikwete kwa watendaji wa serikali na viongozi.

“Maabara hizi 68 tunazojenga zitagharimu kiasi cha Sh bilioni 5.4 hadi kukamilika kwake hivyo tunaomba wadau mbalimbali wa maendeleo na wahisani kutusaidia kama alivyofanya Kampuni ya Mwanza Huduma , si lazima fedha hata vifaa vya ujenzi lengo ni kuhakikisha tunakamilisha ujenzi huu kwa wakati, alisema.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, akipokea msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Konisaga , alimpongeza kwa mchango wake wa kujitolea kutafuta wahisani na wadau mbalimbali kuisaidia Halmashauri ili kukamilisha ujenzi wa maabara ikiwa nia agizo la Rais Kikwete kabla ya mwezi Novemba mwaka huu ambazo ni maabara ya somo ya Phizikia, Kemia na Baiologi.

“Kasi ya ujenzi inaendelea vizuri katika maeneo ya sekondari hizo za Kata zote za jiji ambazo ni Nyamagana, Pamba, Isamilo, Mirongo, Mbugani, Igogo, Mkuyuni, Butimba, Mkolani, Buhongwa, Mahina na Igoma na tulikubaliana katika kikao cha Baraza la Madiwani kuhakikisha tunakamilisha haraka ikiwa kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani na kuomba msaada kwa wahisani na wadau wengine”aliema.

Wito wangu kwa wahisani,wadau mbalimbali kutusaidia ili kukamilisha ujenzi huu na wananchi nao watambue kuwa sekondari hizi ziko kwa ajili ya kuwawezesha watoto wetu kupata elimu bora hivyo na wao waguswe kuchangia kadiri wanavyoweza ili kukamilisha kwa wakati unaotakiwa na kuwapuuza wale wanaowapotosha kuchangia kuwa hawana nia njema na maendeleo yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.