ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 22, 2014

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ASHIRIKI HAFLA YA KUZALISHA TOFALI LA KWANZA LA DHAHABU MGODI WA KWANZA UNAOMILIKIWA NA WATANZANIA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akionyesha tofali la kwanza la dhahabu kuzalishwa na mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO (shirika la kwanza la kizalendo linalomiliki mgodi huo kwa asilimia 99) Balozi Alexanda Muganda. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe (kushoto) wakionyesha tofali la kwanza la dhahabu kuzalishwa na mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa STAMIGOLD akiongoza msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwaonyesha shughuli mbalimbali za uzalishaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo wakiwa katika eneo la uchimbaji ambapo Waziri wa Nishati na Madini nchini amefanya ziara. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo katika ramani ya eneo la uchimbaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo.
Eneo la uchimbaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo.
Uchimbaji ukiendelea.
Shughuli za uchimbaji zikiendelea.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo kwa kina.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongoza msafara kuelekea eneo lililoandaliwa maalum kwaajili ya Hafla ya kusherehekea uzalishaji tofali la kwanza la dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Tanzania inatarajia kuanza kunufaika na madini ya dhahabu baada ya Serikali kuamua kuanza kuchimba madini hayo katika mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tofali la kwanza la dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa uchimbaji huo utasaidia kuongeza ajira kwa watanzania.

Profesa Muhongo ameongeza kuwa hatua hiyo itaondoa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wananchi kuwa rasilimali nyingi nchini zinawanufaisha watu kutoka nje badala ya watanzania.
Kaimu Meneja wa kampuni ya STAMIGOLD Dennis Sebugwao.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kampuni ya STANGOLD  Dennis Sebugwao amesema kuwa Kampuni ya STAMIGOLD  ambalo iko chini ya Shirika la Madini STAMICO inamiliki mgodi huo kwa asilimia 99 huku asilimia 1 ikimilikiwa na Hazina.

Shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwa mgodi huo zilianza mnamo tarehe 2 mwezi julai mwaka huu, huku uendeshaji na shughuli zote za usimamizi na uzalishaji zikifanywa na Watanzania wenyewe. 

Pamoja na mafanikio tuliyonayo bado zipo changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi wetu.
-Kuyumba kwa bei ya dhahabu.

-Tunakabiliwa na ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi huu. Mfano, baadhi ya vitu vinavyohusiana na uzalishaji vingihavipatikani hapa nchini hivyo tunalazimika kuvinunua nje ya nchi kwa gharama kubwa.

-Wavamizi wa mali mbalimbali za mgodi.

-Uhaba wa maji- Tunategemea vyanzo vya maji kutoka Mto Muhama na Isozibi ambavyo havitoshelezi kutokana na matumizi yaliyopo. Mito hii maji yake hutiririka wakati wa mvua tu.

-Ukiritimba katika kupata vibali mbalimbali vinavyohusiana na shughuli za uendeshaji wa mgodi.

-Tupo katika eneo la pembezoni mwa huduma za kijamii hivyo kusababisha kwenda umbali mrefu kwaajiliya kupata baadhi ya huduma za kijamii mfano huduma za matibabu, huduma za kibenki nk.

-Ushindani na makampuni ya madini na hasa makampuni yenye majina makubwa katika kubakiza wafanyakazi wenye utaalamu mkubwa kwani kumekuwa na tabia ya kunyang'anyana wafanyakazi wenye utaalamu na ujuzi wa muda mrefu katika vitengo mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO (shirika la kwanza la kizalendo linalomiliki mgodi huo kwa asilimia 99) Balozi Alexanda Muganda.
Matarajio yetu ni kuwa Mgodi wa kwanza utakaozalisha dhahabu kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu ya Tanzania. Stamigold Company Limited ina matarajio ya kuzalisha dhahabu yenye kiwango cha juu kwa gharama itakayowezesha kuongezeka pato la Taifa kwa muda mrefu wa biashara hii, wakati huo huo kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania na kuvutia washika dau kwa ajili ya maslahi ya taifa zima.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akihutubia katika hafla ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Baadhi ya wafanyakazi katika hafla ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Wadau wa mgodi. 
Ni meza nyingine walipoketi wadau.
Wageni toka mashirika na taasisi mbalimbali wamealikwa kwenye hafla hii ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Wageni.
Mc wa hafla hiyo. 
Wakuu wa idara mbalimbali katika pozi wakifuatilia yanayojiri kwenye hafla ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. 
Sehemu ya wafanyakazi mgodi wa STAMIGOLD.
Kwa umakiiini.... 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifurahia zawadi ya picha aliyokabidhiwa na mgodi wa STAMIGOLD.
Burudani....
Ngoma inogile.
Picha ya pamoja.
Kaimu Meneja wa kampuni ya STAMIGOLD Dennis Sebugwao (kulia) akimsindikiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutoka eneo la hafla ambapo kushoto (mwenye tai nyekundu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.