ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 19, 2014

WAZIRI CHIZA ACHARUKIA WACHAKACHUAJI WA MIZANI YA PAMBA.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia Christopher Chiza (katikati) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kushoto mbele) ambapo nyuma yake amechomoza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wakiingia kwenye ukumbi wa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia Christopher Chiza akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dr. Festus Limbu (Mbunge wa jimbo la Magu) akifuguwa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa salamu za mkoa kwa wajumbe wa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Wajumbe toka mikoa na mikoa, wilaya na wilaya.
Sekretarieti ya Mkutano wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba Kanda ya Magharibi mikoa inayolima zao hilo, katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Tawi la Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dr. Festus Limbu ambaye ni Mbunge wa jimbo la Magu (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wadau wa Sekta ya Pamba.



Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (kushoto) akiwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo wakijadili masuala kadhaa.
Wadau wa Pamba.
NA PETER FABIAN, MWANZA.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia Christopher Chiza, ameiagiza Menejimenti ya Bodi ya Pamba kuwachukulia hatua kali Makamupuni ya ununuzi wa Pamba yaliyofanya uchakachuaji wa minzani wakati wa ununuzi wa pamba musimu wa 2014/2015.

Pia ameliagiza Shirika la Viwango (TBS) pamoja na Wakala wa Vipimo Tanzania kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, wanunuzi wa zao la pamba wanaochakachua mizani kisha kuwaibia kilo wakulima wa pamba.

Waziri Chiza aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 11 wa wadau wa Sekta ndogo ya Pamba, uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Mwanza kisha kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya, wabunge, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri na wadau wengine.
 Alisema TBS pamoja na Wakala wa Vipimo nchini wanao wajibu wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wafanyabiashara wote wa zao la pamba wanaotumia mizani mibovu, na kwamba huo ni wizi usiovumiliwa na serikali.

Waziri Chiza alisema kumekuwepo na tabia chafu ya wanunuzi wa pamba kuwaibia wakulima, rasilimali yao hiyo kinyume cha sheria, na kwamba la kudhibiti wizi huo hawezi kulifanya yeye kama waziri bali mamlaka husika za Wakala wa Vipimo na TBS.

“Wengine wananipigia simu mimi ili nidhibiti mizani iliyochakachuliwa, kimsingi mimi ni kiongozi wa juu siwezi kufanya hivyo, wapo TBS na Wakala wa Vipimo ambao ndiyo wenye mamlaka ya kudili na watu kama hawa.

“Lakini pia nakiri kwamba serikali haijawahi kuchangia fedha kwenye mfuko wa kuendeleza zao la pamba, ingawa ni mdau mkubwa wa sekta hii. Kwa hiyo serikali inaiagiza Bodi ya Pamba ihakikishe tatizo la mbegu za pamba zisizoota lisijitokeze tena,” alisema Waziri huyo wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

Katika hatua nyingine, waziri huyo alisema serikali inaandaa utaratibu wa kuanza kuwalipa fidia wakulima walioathirika na mbegu za pamba ambazo hazikuota kwenye mashamba yao, licha ya kuuziwa na wadau.
Kuhusu kuvunjwa kwa uongozi wa Bodi ya Pamba, Waziri Chiza, alisema serikali kupitia wizara yake ipo kwenye mchakato maalumu wa kuhakikisha viongozi wengine wapya wa bodi hiyo wanapatikana, kwa lengo la kusimamia Sekta ndogo ya Pamba.

“Naomba niweke kumbukumbu sawa katika mkutano huu ambao upo kisheria. Bodi ya Pamba imeshamaliza muda wake, na wizara yangu inafanya mchakato wa kupata viongozi wengine kwa ajili ya kusimamia Sekta ndogo ya Pamba,” alisema Waziri Chiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo wa wadau wa zao la pamba, Dk. Limbu alisema Bodi hiyo ya Pamba inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha za uendeshaji wa sekta hiyo ndogo kwa wakulima kote nchini kutokana na serikali kutwasilisha mchango wake katika Mfuko wa kuendeleza zao la Pamba (CTDF) kwa wakati.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist Ndikilo aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo wa 11 wa Sekta ndogo ya Pamba kwamba, mkoa huo unashika nafasi ya pili kitaifa kwa kulima zao la pamba ukiongozwa na Mkoa wa Simiyu, hivyo aliomba zao hilo litiliwe mkazo ili kuleta maendeleo kwa jamii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.